ZITTO KABWE ATIMIZA AHADI YAKE.... ATAJA MSHAHARA WA RAIS KIKWETE

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania analipwa sh milioni 384 kwa mwaka, sawa na sh milioni 32 kwa mwezi pasipo kukatwa kodi.

Hii ni mara ya pili kwa Zitto kutangaza hadharani mishahara ya viongozi wakuu wa serikali, akiwa ameanza na ule wa Waziri Mkuu, aliyesema analipwa takribani sh milioni 26 kwa mwezi.
  
Akiwahutubia wananchi mjini Igunga jana, ukiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kuimarisha chama Kanda ya Magharibi, Zitto ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Kaskazini alisema kuwa sababu ya kutaka mishahara ya viongozi wakuu wa nchi ijulikane, ni kuzuia mianya ya watu wachache kuiibia nchi kutokana na usiri wa jambo hilo.
  
Zitto alisema hoja ya msingi si kiasi wanacholipwa viongozi hao walioajiriwa na wananchi, bali ni usiri unaofanywa juu ya kiwango hicho jambo alilosema kuwa linaweza kutumiwa na wajanja kuendelea kuinyonya nchi.
  
Alisema ni jambo la kusikitisha kuona mwalimu anayelipwa mshahara wa sh 220,000 kwa mwezi akikatwa kodi, huku viongozi wa kuchaguliwa wakiwa wanapokea mishahara mikubwa pasipo kukatwa kodi licha ya kuhudumiwa kila kitu na serikali.
  
Aliongeza kuwa katiba ya sasa Ibara ya 43(1), inaeleza kuwa rais atalipwa mshahara pamoja na malipo mengine, huku ibara hiyo hiyo kifungu cha pili ikizuia mshahara na marupurupu kupunguzwa, hali aliyoelezea kuwa ni muhimu katiba mpya ikabadilisha sheria hizo kwa manufaa ya nchi.
  
“Kwa hiyo hata kesho kama Dk. Willibrod Slaa akiwa rais na akataka kupunguza mshahara wake, kwa katiba hii hawezi na hili jambo si sahihi kwani viongozi wa ngazi hizi wanapata kila kitu bure kutoka serikalini,” alisema Zitto.
  
Akiwa katika Kata ya Choma, Zitto alikagua kilichokuwa kiwanda cha kuchambulia pamba cha Giner ambacho kimeacha kufanya kazi tangu mwaka 1998.
  
Alisema kufa kwa viwanda vingi vya uzalishaji nchini kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na Serikali ya Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, akidai kuwa alishindwa kutofautisha suala la uwekezaji na biashara huru.
  
“Ni serikali ya Mkapa ndiyo ilitufikisha hapa katika kupotea kwa viwanda nchini, wao walidhani biashara huru ni kuwapa wawekezaji viwanda vyetu na serikali kujiweka pembeni, sasa nchi imebaki kutegemea uchumi wa uchuuzi badala ya uzalishaji,” alisema.
  
Alisema sera ya uwekezaji katika Serikali ya CCM ilichukuliwa kama fursa ya viongozi wa chama hicho kujinufaisha na mali za serikali pasipo kujua wataendeleza vipi.
  
Zitto alisisitiza kuwa kila mara CHADEMA imekuwa ikisisitiza bungeni juu ya kupiga marufuku usafirishaji wa pamba kwenda nje kama malighafi, na badala yake wakitaka viwanda vifufuliwe kwa ajili ya kutoa ajira kwa Watanzania.
  
Alirejea kusisitiza sera ya hifadhi ya jamii kwa wakulima akisema imefikia wakati serikali kupitia SSRA ione umuhimu na ulazima wa kuhakikisha wanaongeza Watanzania wenye hifadhi ya jamii kwa kuanza mfumo maalumu wa hifadhi ya jamii kwa wakulima (Supplementary scheme for social security to small holder farmers).
  
“Ninapendekeza serikali ichangie nusu kwa nusu na mkulima ili kuvutia uwekaji akiba katika nchi na kuwa na sera ya uwekezaji katika maeneo yatakayomwinua mkulima kama miundombinu ya umwagiliaji, mikopo nafuu kwa wakulima kwenye pembejeo na nyumba na bima ya afya.
  
“Nimezungumzia umuhimu wa uwazi katika matumizi ya fedha za umma ikiwemo malipo ya watumishi na viongozi wa umma. Nimewaeleza wananchi wa Nzega kuwa siku ya Jumanne kamati yangu ya Hesebu za Serikali (PAC) itaanza kukagua mahesabu ya vyama vya siasa nchini,” alisema.
  
Zitto alisema vyama vya siasa vinatumia fedha za umma takribani sh bilioni 20 kila mwaka kama ruzuku, kwamba ni haki ya wananchi kujua fedha zinatumika namna gani.
  
Alisema kuwa wananchi wa Nzega wana changamoto nyingi sana. Kwamba wakulima wa pamba walipewa madawa feki ya kuua wadudu, michango ya hovyo hovyo ni mingi mno na unyanyasi wa wana-CHADEMA ni mkubwa vijijini.


-Tanzania  Daima 


Udaku Specially Blog
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

19 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Asante kaka kwa kutufumbua macho

    ReplyDelete
  2. Inatisha sana,huu ni unyonyaji uliokithiri,endelea jembe letu

    ReplyDelete
  3. Dah! Hii kali, inakatisha hata tamaa kama mwalimu ndio kipato chake.

    ReplyDelete
  4. Na ndio maana Walimu hauwajali Mh Raissssssssss,ila poa kila mbuzi anakula urefu wa kamba yake

    ReplyDelete
  5. Na ndio maana Walimu hauwajali Mh Raissssssssss,ila poa kila mbuzi anakula urefu wa kamba yake

    ReplyDelete
  6. Hii nchi ye2 2naenda wapi txatxa? duuh!

    ReplyDelete
  7. Rais wetu gold-digger!

    ReplyDelete
  8. Huu mshahara ni mdogo sana, ni pungufu mara 81.25 ya mshahara wa Lionel Messi kwa mwezi. naona angalau wangempa hata million 100 hivi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nimekupendaje...

      Delete
    2. nyie wawili hapo juu sio wazima. Mkapimwe akili! Angalia tofauti iliyopo kati ya mshahara wa Mwalimu na Rais.

      Delete
    3. kwani mwalimu raisi,uctake kulinganisha mwanga jua na wa tochi..@ rwabukambara

      Delete
    4. Aisee mdau umefail kutofoutisha bomu na ushuz...Hahahahaaaa@ swtbrt

      Delete
  9. Iyo mil 100 walipwe waalimu mavi nyie

    ReplyDelete
  10. nanyie jitahdin muwe rais mpate huo mshahar, fanyeni kaz achen kukalia hay nafs ipo 2015 na 2020

    ReplyDelete
  11. Dah ndio maana wanaiba rais ajae apewe ata 200, 000, 000/= kwa mwezi

    ReplyDelete
  12. Safi kaka zito endelea kuwa mkweli.mungu atakulipa.nimesikitika sn na mshara anaopokea mwalim then kikwete anakula 36 kwa mwez tena bila kukatwa kodi.hawa jamaa wanazambi sn kwa mungu

    ReplyDelete
  13. Hana uchungu na nchi anachuma asepe sijui ntampata wapi niwe hata mke wa tatu?

    ReplyDelete
  14. YOU know what, unyonyaji hautoki nje, ni sisi wenyewe ndani ya nchi. hii si haki kabisa. Katiba kwa nini isibadilishwe hilo eneo la mishahara, kwani hiyo katiba imeandikwa na nani si ni watu. tukiwa na viongozi Imara wanaojali wanadamu wezao ni lazima atasimamia hiyo katiba na kubadirishwa na kuwafanya wananchi anao waongoza nao wanapata pato la kukidhi mahitaji yao kama wanadamu wa kawaida.

    ReplyDelete
  15. dawa ni hivi, hakuna uchaguzi mwaka 2015 mpaka hiyo katiba irekebeshwe tena na mengine mengi yanayohitajika kuibadirishwa kwa manufaa ya wananchi wote. haki ni usawa.wapiga kura na wapigiwa kura na washindi na washindwa wote ni wanadamu haki ni sawa.

    ReplyDelete

Top Post Ad