TAARIFA YA KUKATIKA KWA MAWASILIANO YA VODACOM‏

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Dar es Salaam, 5 Februari, 2014.Tunapenda kuwaomba radhi wateja wetu wote kwa kushindwa kutoa huduma za mawasiliano kuanzia asubuhi ya Februari  5, 2014. Hii imetokana na kukatika kwa mkonga wa mawasiliano ulioko barabara ya Morogoro na  nyingine mbili za ziada zilizoko Mlalakuwa na Mayfair plaza barabara ya Mwai kibaki jijini Dar es Salaam.
Kukatika kwa Mkonga huo kumesababisha vituo vyetu vya kutoa huduma za mawasiliano vilivyopo Oysterbay na mbezi juu kushindwa kufanya kazi kutokana na vituo hivyo kutegemeana kumesababisha kushindwa kutoa huduma za mawasiliano.
Kutokana na hilo wateja hawakuwa na uwezo wa kupiga simu, kutumia intaneti na hata  huduma za kifedha. Tunatambua usumbufu ambao umetokea kwa kukosa mawasiliano, kwa mara nyingine tena tunaomba radhi na tunashukuru kwa uvumilivu wao katika kipindi chote ambacho huduma zilikosekana. 
Mafundi wetu wameweza kurekebisha uharibifu uliotokea barabara ya Mwai kibaki ambao uliotokana na shughuli za ujenzi  wa barabara zinazoendelea. Uharibifu mwingine uliotokea katika Barabara ya Mlalakuwa ulichukua muda kurekebisha kutokana na nyaya zilizo katika mkonga wa mawasiliano kuungua kulikosababishwa na zoezi la uchomaji taka lililokuwa linaendelea katika sehemu ambayo mkongo umepita na kusababisha uharibifu huo. 
Napenda kuwahakikishia wateja wetu kuwa, Tumejidhatiti katika kuendelea kutoa huduma bora na za kipekee  wakati wote watakapokuwa wanautumia mtandao wa Vodacom, Tunawashukuru kwa namna ambavyo wameendelea kutuunga mkono na kutuvumilia pale matatizo yanapojitokeza. 
Rene Meza 
Mkurugenzi Mtendaji – Vodacom Tanzania
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. U dont need yo tell us blah blah hapa.tulipe fidia kwa usumbufu tulioupata.maana wengine wamefiwa na ndugu zao simply kwa kushindwa kuwatumia fedha za matibabu through Mpesa na wengine wamegombana na familia zao kwa kushindwa kuwa hewani.useless Tanzanian service providers!!! Simple statement umemaliza!!!real????

    ReplyDelete
  2. kawaida sana hakuna haja ya kulaumu

    ReplyDelete
  3. hata hivyo ilikuwa poa sana maana waliokuwa na miadi ya kuvunja amri ya sita walikwama

    ReplyDelete

Top Post Ad