Baaya ya Brazil Kumtimua Kocha Capello Huyu Ndio Kocha Mpya wa Team Hiyo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Shirikisho la soka la Brazil CBF limemtangaza aliyekuwa mchezaji wa Brazil Dunga kuwa kocha wa timu ya taifa kwa mara ya pili.
Dunga aliyeiongoza Brazil kutwaa kombe la dunia la mwaka wa 1994 aliwahi pia kuwa kocha katika mwaka wa 2006 hadi 2011.
Dunga amechukua pahala pake Luiz Felipe Scolari, ambaye alijiuzulu kufuatia kimbunga cha mabao 7-1 ambayo timu hiyo ililazwa na Ujerumani katika hatua ya nusu fainali .

Sadfa ni kuwa Kocha huyo mwenye umri wa miaka 50 naye alifutwa kazi baada ya selecao kubanduliwa nje ya kombe la dunia la mwaka wa 2010 katika hatua ya robo fainali.
Carlos Alberto Parreira ndiye aliyechukua pahala pake lakini hata naye haku dumu Scolari alipotajwa kuwa Kocha.
Scolari mwenye umri wa miaka 65 aliiongoza Brazil katika semi fainali za kombe la dunia ambapo timu hiyo ilipata kichapo kibaya cha mabao masaba kwa moja dhidi ya mabingwa wa kombe la Dunia Ujerumani.

Dunga amewapiku mkufunzi wa kilabu ya Corinthians Tite,Mkufunzi wa kilabu ya Sau Paulo Muriciy Ramalho na Vanderlei Luxembourg ambaye aliwahi kuifunza timu hiyo kutoka mwaka 1998 hadi mwaka 2000.
Wakati huohuo kocha wa Argentina Alejandro Sabella, 59, amesema kuwa atatangaza hatima yake juma lijalo baada ya kushindwa bao moja kwa nunge na Ujerumani katika fainali ya kombe la dunia huko Brazil mapema mwezi huu .
Wachezaji wanamtaka kocha Sabella kuiongoza timu hiyo katika kipute cha kuwania ubingwa wa mataifa ya Amerika ya Kusini yaani 2015 Copa America mashindano yatakayoandaliwa huko Chile.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mdaku angalia kichwa chako cha habari.

    ReplyDelete
  2. Capelo?? Umekosea brazil kocha alikua abdalah king kibaden... hongera dunga ila fukuza fred fukuza paulinho waite andry coutinho na jaja wa yanga.. utachukua copa america comfederation world cup mpaka euro ka watakualika!!

    ReplyDelete
  3. Captain Dunga is baaaaaccckkkk

    ReplyDelete

Top Post Ad