Mgombea Udiwani 2015 Anaswa Kitandani Akiwa na Mwanafunzi Guest House

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

HILI nalo janga! Mwanaume mmoja anayesemekana ni mfanyabiashara ambaye pia anatajwa kugombea udiwani wa kata moja iliyopo  Kinondoni jijini Dar es Salaam, aliyetajwa kwa jina moja la  mzee Beno amenaswa akiwa chumba cha gesti na denti wa chuo kimoja kilichopo Kibamba jijini Dar, Ijumaa ‘kubwa’ lina mkanda wote.

Tukio hilo la aina yake lilijiri Oktoba 20, mwaka huu ndani ya gesti moja (jina tunalo) iliyopo Kimara-Suka jijini Dar es Salaam ambako mama mzazi wa wa binti huyo ndiye aliyemnasa mheshimiwa mtarajiwa huyo na binti yake.

WASIWASI KWANZA
Awali, mama huyo alisema  alianza kuwa na wasiwasi na mwenendo wa binti yake huyo kutokana na kuanza kale katabia ka’ kuchelewa mara kwa mara kurudi nyumbani akitoka chuoni, akajiongeza!
“Sisi tulishajua binti yetu ameanza katabia kabaya, akienda shuleni anachelewa kurudi wakati si kawaida yake, tukasema kuna jambo linaendelea kwake,” alisema mzazi huyo.

USHUSHUSHU 
Kwa mujibu wa mzazi huyo aliyeonekana kufura kupita tafsiri ya neno lenyewe, alianza kibarua cha ushushushu kama si upelelezi wa kumfuatilia binti yake ambapo siku moja aliifanyia udukuzi simu yake na kukuta ujumbe mfupi wa maneno  (SMS) kwenye simu hiyo ukimtaka afike kwenye gesti hiyo.

MBALI NA UJUMBE
Ikadaiwa kuwa, mbali na SMS hizo, mama huyo aliwahi kumsikia binti yake akiwa hewani na ‘mheshimiwa’ huyo jambo lililozidisha hasira zake kama mama akiamini kuna mwanaume anamharibu binti yake aliye na malengo naye mazuri siku za usoni.

BINTI ATII AMRI YA WAZAZI
Ndipo mama huyo akamuweka kikao kifupi binti yake na kumtaka aseme ukweli kuhusu mtu aliyemuita gesti Kimara-Suka.

NI KAMA WALISEMA
“Mtu gani mama?”
Mama: “We’ usinitanie, nimekuta meseji kwenye simu yako, kuna mwanaume umemsevu kwa jina la Sweet, amekuita gesti, ni nani?”
Binti: “Aaah! Ni mzee mmoja hivi.”
Mama: “Anaitwa nani?”


Binti: “Anaitwa mzee Beno.”
Mama: “Ni mpenzi wako?”
Binti: (moyoni) “mama bwana, sasa si umeona nimemsevu Sweet anaweza kuwa mjomba ‘angu kweli?  (kwa sauti) “ndiyo mama lakini sijawahi kufanya naye chochote hata siku moja.” 
Mama: “Apia.”
Binti: “Hakyamungu vile.”

MTEGO
Ikadaiwa kuwa baada ya hapo, binti akatakiwa kumjibu mzee huyo kwamba anakwenda wakutane huko gesti ili  wamalizane kwani ‘amemmisi’ sana siku hiyo, mzee akashindwa kujiongeza. 
Binti akiwa na mzazi wake na skwadi nyingine walianza safari ya kwenda Kimara –Suka kwenye gesti hiyo ambapo walikaa baa ya jirani, binti akaenda ndani ambako mzee huyo alishafika zamani gani na kumsubiri.

Baada ya muda, binti alituma meseji kwa mama yake akisema mambo tayari, wapo ‘weupe pee’ (hawana nguo). Ndipo mama huyo akachukua timu yake na kuvamia gesti hiyo kwa ajili ya kulianzisha.

OFM YAKATIZA MITAANI, YAKUMBANA NA KASHESHE
Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ya Global Publishers ilikuwa ikikatiza mitaani kusaka matukio kwani ni ada yake, ndipo walipoibukia eneo lenye gesti hiyo na kukumbana na kasheshe hilo la nguvu.
 “Hawa wazee ndiyo wale ambao wanaharibu watoto wa watu huku yeye wanawe wakisoma vizuri na hakuna anaowaharibia masomo yao,” alisikika akichonga mama huyo.
Akaendelea: “Jamani nawaomba njooni na makamera yenu yote hapa.”

OFM YAPATA NGUVU
Kufuatia maneno ya mama, OFM walipata nguvu na kuanza kupiga picha za kumwaga kwa ajili ya kumbukumbu.

MGOMBEA ASEMA NENO
Huku akiwa amekaa kwa tafakuri ya kina, mzee Beno alisema ameumbuka na kuitaka familia ya mwanafunzi huyo kumalizana kifamilia nje ya gesti hiyo huku akiwaomba OFM chondechonde wasiitoe habari gazetini.

Hata hivyo, mpaka tunakwenda mitamboni, mwanamke huyo alisema hawajamalizana chochote hivyo OFM inaendelea kufuatilia sakata hilo.
~Credits:GPL
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mwanafunzi ana miaka mingapi? Kama 18 au zaidi ni jukumu la mke wa beno kufumania.

    ReplyDelete
  2. Hmmm hata kama ana miaka 18 ni mwanafunzi, tena yeye diwani muwakilishi anagombania, na mwanafunzi wapi? na wapi? hmmm ndio uongozi huu, atawakilisha nini? katika jamii,

    ReplyDelete
  3. Umeumbuka! Mungu katuonyesha kwamba hufai kuwa kiongozi.
    Au na wewe utatuambia kuwa ni wapinzani ndani ya chama chako kama mzee mtemvu?
    kama ni mwanao angefanyiwa hivyo si kazi ungeua mtu,mbegesiiiiiiii

    ReplyDelete
  4. mwanafunzi wa chuo bado unamfuatilia hujui nayeye anapata hamu ya kutiwa au wewe mama ulitaka umtomb.e wewe. huyo mchukue sasa mkasagane, baada ya muda hayo yataisha atapatikana kidume mwingine atamtomb.a kama kawa. shiiit!

    ReplyDelete
  5. Hiyo ni kisiasa zaidi huyo demu kapangwa amuharibie huyo baba kwenye uchaguzi ila na yeye akome kutongonza dogo dogo.

    ReplyDelete

Top Post Ad