Diamond Platnumz Agundua Dawa ya Wazomeaji Katika Show zake, Wazomeaji Wageuka Ghafla na Kuanza Kumshangilia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Msanii  anayetesa  katika  mziki  wa  kizazi  kipya  hapa  nchini, Nassib  Abdul  'Diamond  Platnumz'  usiku  wa  jumamosi  iliyopita  alijikuta  katika  wakati  mgumu  baada  ya  kuzomewa  na  mashabiki  kwenye  viwanja  vya  Leaders  Jijini  Dar  es  Salaam.

Mbali  ya  kuzomewa, Diamond  pia  alirushiwa  chupa  za  maji  ambazo  zilileta  kadhia, lakini  Diamond  alionekana  akiwahimiza  madancer  wake  wafanye  kazi  iliyowapeleka  pale  licha  ya  zomeazomea  kuzidi  uwanjani.....

Msanii  huyo  alipoona  vitendo  vya  kutaka  kumkwamisha  asiimbe  vikiendelea, aliamua  kuwamwagia  fedha  mashabiki hao, ndipo  wakaacha  kuzomea  na  kuanza  kugombea  fedha  hizo  kisha  kuanza  kumshangilia....

Baadhi  ya  wadau  walisikika  wakidai, kundi  hilo  lililokuwa  likimzomea  liko  upande  wa  mmoja  wa  wasanii  mahiri  hapa  nchini.Wasanii  wengine  walioonja  joto  ya  jiwe  ni  pamoja  na  Khamis  Mwinjuma  'Mwana FA'  na  Ambwene  Yesaya  'AY'.

Aidha, baadhi  ya  mashabiki  walilaani  vikali  tukio  hilo  la  kumzomea  Diamond  na  kumrushia  chupa  za  maji  ambazo  inadaiwa  zilikuwa  na  haja  ndogo  ndani  yake.

Mashabiki  hao  walisema  tukio  hilo  halipendezi  na  linapaswa  kukemewa  na  kuwataka  waratibu  pamoja  na  jeshi  la  polisi  kuzidisha  ulinzi  katika  matamasha  makubwa  kama  hayo.

Hii  ni  mara  ya  pili  kwa  Diamond  kuzomewa,tukio  la  kwanza  likiwa  kilele  cha  tamasha  la  Fiesta  mwaka  jana  kwenye  viwanja  hivyo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hao watu wa Udaku njoo wanamfanya Diamond azomewe.

    ReplyDelete
  2. OK, kwahiyo kila atakapo zomewa atakuwa akimwaga pesa. Kama Domo kagundua dawa ya wazomeaji na kumbe na wazomeaji nao wamegundua dawa ya kupata pesa - ngoma droooooooooo!!

    ReplyDelete
  3. Hata wafanye nini bado nyota ya nguli hiyo imo juu,,kama maulana amepanga hakuna atakayepangua.....mwisho walila kwa diamond au makao....watu wasio na la kufanya ndio wanayoyafanya hayo....fools always remain fools....Diamond bado atapanda tu mpende msipende....ni wakati wake ngoje wake wenu ama waambulie tu kuzomea na kwenda kushi vichumba vya kupanga....

    ReplyDelete
  4. Nyie ndio mnataka sasa azomewe kila show watu wakitaraji kurushiwa pesa

    ReplyDelete
  5. Acha tuzomèe tupate nauli

    ReplyDelete
  6. Tatizo la watanzania ni ushamba umetuzidi, badala ya kuwapa support wasanii wetu wanaotuwakilisha vizuri nje ya nchi eti tunazomea kwa kumfurahisha mjinga mmoja aliyeshindwa music na kutafuta soko la kimataifa. Huyo kima wenu anatakiwa akubali matokeo kuwa muda wake ulishapita alishindwa kuitumia nafasi yake, sasa hivi akae pembeni ausome tena mchezo unaendaje na kuongeza bidii kwenye game siyo kutafuta watu wa kuzomea, hiyo haisaidii, kwani wazomeaji wote ni wale mamburula wasiojielewa. Ni hayo tu, mtake mistake Domo kawadizi na kuzomea siyo dawa, someni mchezo mwenzenu anafanyaje hadi kafika hapo, punguzeni wivu nyie bongo flevar na njama zenu za kishamba.

    ReplyDelete
  7. hahahahaaa we bwege hapo juu unalalamika hadi unatia huruma
    inaelekea domo anajupumuliaga vizuri kisogon

    ReplyDelete
  8. hahahahaaa we bwege hapo juu unalalamika hadi unatia huruma
    inaelekea domo anajupumuliaga vizuri kisogon

    ReplyDelete

Top Post Ad