Askari Polisi wa Kike Avuliwa Nguo na Kuachwa Mtupu, Watu Wanane Wafikishwa Kortini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wafanyabiashara watatu na wanachuo watano wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida wakikabiliwa na mashitaka ya kumdhalilisha kupindukia askari polisi wa kike na kumsababishia maumivu makali mwilini.

Mwanasheria wa Serikali, Petrida Mutta alidai mbele ya Hakimu Joyce Minde, kwamba kwa pamoja, washitakiwa hao walimfanyia unyama askari huyo kwa kumvua nguo zote na kumwacha mtupu kisha kumshambulia na kumsababishia maumivu makali mwilini.

Waliopandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi, Joyce Minde, ni Jasmin Iddi (40), Abdallah Hamduni (26), Ramadhani Bakari (32) wote wafanyabiashara wa mjini hapa pamoja na dereva, Saidi Saidi (50) .
Wengine ni Aurelia Adolf Mushi (20), Grace Daniel Paul (21), Happiness Kiluvya (23), Jackline John (20) na Constansia Masaki (21) wanaodaiwa ni wanachuo katika moja ya vyuo vya elimu ya juu mjini Singida.

Mwanasheria wa serikali, alidai wakati wote wa kitendo hicho cha udhalilishaji, polisi huyo, alikuwa akichukuliwa picha za video huku akiwa mtupu na kuzisambaza kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Tukio hilo inadaiwa lilifanyika Februari 14, mwaka huu saa 11.30 jioni ambako kwa mujibu wa Mwendesha Mashitaka, inadaiwa polisi huyo wa kike alikutwa akiwa na mume wa mshitakiwa, Jasmin wakiwa kando ya Ziwa Singidani wakivinjari siku hiyo ya Wapendanao.
Hata hivyo, mume ambaye jina halikupatikana, inadaiwa alitoroka. Mutta alidai mbele ya mahakama hiyo kuwa kitendo walichofanya washitakiwa ni kinyume na Kanuni ya Adhabu 138 A kifungu cha 16 cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai kama kilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002. Wote walikana mashitaka
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

14 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. KWELI SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE WAPEWE ADHABU KALI SANA KWANI INASITIKISHA NIIONA HIYO VIDEO KWA KWELI NI MBAYA MNOO.

    ReplyDelete
  2. Hiyo CLIP NIMEIONA KWA UFUPI SIO VIZURI KABISA KUMVUA NGUO

    ReplyDelete
  3. Kwa vile ni askari ndio achukue mume wa mtu! Acheni kutumia vibaya dhamana mliyopewa, hata ukiwapeleka mahakani ukweli unabaki UMESHAADHIRIKA na KUDHALILIKA kweupeee. Pumbavu kabisa kuendekeza KINDUMBWENDUMBWE tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na wahusika lazima( LAZIMA ) wataenda kunyea ndoo(,tunahakikisha iwe hivyo.)Sasa ipi kubwa kuliko nyingine?kufungwa?au kuvuliwa nguo?

      Delete
  4. HATA WAKATAE PICHA ZAO TUMEPATA KWENYE WHATS UP BINAFSI SIKUPENDA .SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE

    ReplyDelete
  5. WAPEWE ADHABU KALI SANA!!!

    ReplyDelete
  6. picha hata sasa ninayo kwenye cm iliniuma sana kuona mtu akibuluzwa na kuvuliwa nguo mbele ya wanaume ten binafsi nilifikili ni hapa dar baada yakuona bahari kumbe ni ziwa singida. sasa glob mnaficha nini

    ReplyDelete
  7. HIVI KUMDHALILISHA MWANAMKE MWENZIO HIVO NININI AU UNAFIKIRI UMEZALIWA KWA AJILI YAKE TU. HAINOGI HIYO UKILA KILA SIKU!!!!! LAZIMA ATOKE UKITAKA NA WEWE CHEPUKA TENA YULE DADA ALIVAA HIJABU MWEUPE ANAONEKA NAYE ALISHAGAWA SANA SASA KATULIA SASA INAUMA EEH

    ReplyDelete
  8. NA KULIKUWA NA MIDUME KIBA MINGINE IKAWA INAMSAIDIA KUMVUA MINGINE INASEMA MWACHE TU NA NGUO APANDE KWENYE GARI

    ReplyDelete
  9. HIVI MLIVOIRUSHA MLIZANI MNAKOMESHA SANA LAKINI MLIACHA USHAHIDI KWANI DADA MMOJA NAFIKIRI NDO MHUSIKA ALIONEKANA SANA AMEVAA NGUO NYEKUNDU HIJABU YA BLUE BAHARI NA ALIYEFUMANIWA KAVAASURUARI YA KIJANI

    ReplyDelete
  10. HUO NI UONEVU, HAKUMFUMANIA NA MUMEWE BALI WALIKUWA WAMEKAA WAKIVINJARI PEMBEZONI MWA ZIWA SINGIDANI JE IWEJE AMTENDEE HIVYO TENA MBELE YA WATU. KIBAYA ZAIDI WAMEMPIGA PICHA ZA VIDEO NA KUZISAMBAZA SANA HATA MIMI NILITIMIWA . SHERIA IFATE MKONDO WAKE.

    ReplyDelete
  11. SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE ALICHOFANYA NI KIBAYA MNO YULE DADA HAFAI KATIKA JAMII. ATAWAVUA WANGAPI NA MUMEWE NI KIWEMBE?? ANA KAROSO HUYU MAMA MAANA KWA JINSI ALIVYO UKIMLINGANISHA NA YULE ASKARI UNASHANGAA KWANINI KAACHWA HOME NA MUME KWENDA KULA VALENTINE NA YULE ASKARI. MAMA JIULIZE!!!

    ReplyDelete
  12. AVULIWE TU TUMECHOKAA

    ReplyDelete
  13. SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE TAFADHALI

    ReplyDelete

Top Post Ad