Andiko Hili la Wema Kuhusu Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015, Laungwa Mkono na Wengi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Naomba mimi kama Wema Sepetu, nitoe tamko langu rasmi kuhusu hii Sheria mpya iliyopitishwa bungeni. Naongelea Sheria ya cybercrime au cyberbulling. Ukweli ni Kwamba watanzania tunatumia vibaya mitandao ya kijamii. Matusi yamekuwa ni mengi na sometimes hawavumiliki. Kwa kweli kunahitahija Kuwa na laws in place za kupunguza unyanyasaji kupititia mitandao ya kijamii. That said, yes nai support hii bill ya cyber crime to an extend.

Kama jinsi ambavyo watanzania tunatumia vibaya mitandao kwa kuumizana kwa njia ya matusi na kuchafuana, wana siasa wetu waliopitisha hii Sheria ya cybercrime pia wameitumia vibaya hii Sheria na kuitumia kama silaha ya kumfunga mdomo mtanzania.

Kusema ukweli mimi kama Wema Sepetu nimechoka kutukanwa, mpaka mama yangu mzazi anadhalilishwa humu Kwenye mitandao. Kuna kipindi nilifikia hatua ya kuwaza bora nife tu ili kuepukana na matusi na kuandikwa na magazeti kwa habari za uongo.

 Lakini as much as ningependa Kuwe kuna Sheria kama hii ya kunisaidia mimi Wema niepukane na matusi Naona ni bora niendelee kutukanwa mpaka Siku nitakayokufa kuliko kuona fans wangu mimi, fans wa Wolper, fans wa Jokate, fans wa Ali Kiba, fans wa Diamond Platinumz na Wengine wengi wakinyang'anywa haki yao ya msingi kabisa ambayo ni haki ya kuweza kufungua mdomo na kuongea hata yale ambayo sisi mastar na wanasiasi hatukubaliano.....Je mimi kama Wema nitasemaje nawadhamini fans wangu ambao wao ndo wamenipa umaarufu huu na kunifikisha hapa nilipo kama hapo hapo nitawanyanyasa kwa kuwapokonya haki yao ya freedom of speech.

Mimi Wema sijakamilika , wote mnajua ninamapungufu yangu , je mimi Wema nitawezaje kujua makosa yangu ili niweze kubadilika na kufanyA vizuri kama sitokubali kusikiliza maoni ya watu wote yawe mabaya au mazuri?Nafikir wore mnajua hakuna page ya Mtanzania hapa instagram yenye matusi na malumbano kama page yangu mimi ....

Nimeshauriwa sana Kuwa nianze kublock wote wanaoniwekea comment za matusi na kufuta comments zao kama wanavyofanya mastaa wengine lakini nimegoma. Je mnadhani mimi nafurahia hizo comment za matusi? Tena Kwenye page yangu mwenyewe? Hapana zinaniumiza ila pia nakumbuka Kuwa mimi ni kioo cha Jamii nakumbuka Kuwa kabla ya Wema sepetu first comes nchi yangu .....

Niko tayari nitukanwe lakini haki za fans wangu, haters wangu na watanzania wote kwa ujumla ziwe po pale pale. Watanzania naomba tuungane katika kumsupport my dada Kwenye hili @iworeadress @iworeadress. Mimi nimemwelewa sana anachokisema. Tunaelekea pabaya Sasa....Tupiganie haki zetu za uhuru wa kuongea. Tusipojipigania hakuna wa kutupigania. Naamini Chama changu nachokipenda cha CCM kitatusikukiza wananchi wake na kufanyia hilo kazi.Tafadhali follow hii page ili tuweze kuchangia na kabadilishana mawazo . @ccmchangeorquit

By Wema Sepetu on Instagram
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwaiyo waachwe waendelee kutukana au watoe maon bila matus cjamuelewa madam kwakwel

    ReplyDelete
  2. Na nyinyi kina Wema na mnaaojiita mastaa wa Bongo muvi, kwani mnakera sana mnapotupa mapicha zenu mitandaoni mkiwa nusu uchi na maneno ya kebihi,, ama sivyo mtazidi kutukanwa tu hata kama sheria itapitishwa, sheria zimewekwa kuvunjwa, kwa hiyo usifikilie kwamba sheria itawekwa kwa wale wanaotoa matusi kwenye mitandao, hata nyiyi manao weka uchi zenu kenye mitandao,,, kwa hivyo hiyo barua yako kabla hujaipost itupe chooni.. mjirekebishe kwanza tuone kama utatukanwa!

    ReplyDelete
  3. Sasa hicho alichokiandika ndio kitu gani. It doesn't make sense kabisaaaaaa..........hata mtoto wa Darasa la Tatu anaweza kujua nini cha kuandika na jamii ikamuelewa.

    ReplyDelete
  4. nyie manony wote zero brain kasomeni kwanza sheria yenyewe ndo muanze kuchambua watu wanaoipinga.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe mwenyewe umeisoma? Ama wewe ndo mwanasheria asieenda shule? isome kwanza wewe alafu nasi tutafuata nyuma..maana umetuona hatujui kusoma.

      Delete
  5. hivi huyu wema shughuli zake halisi ninini hapa mjini? naomba wadau mnijibu? au kipato chake kinatokana na kufanya shughuli gani?

    ReplyDelete
  6. Hii kitu ya followers ndio inamzuzua. Haingii akilini mtu anaona ni poa tu kutukanwa eti kisa Funs wake wawe na uhuru!!!

    ReplyDelete
  7. Binafsi nimemuelewa Wema vizuri sana, anachokitetea ni UHURU WA KUTOA HABARI. Kwamba yeye hata fans zake ambao wanamtusi hawafuti kwenye page yake kwa kuwa ni mojawapo ya kupata taarifa zinazomhusu yeye kama Wema, ni kweli wanatukana lakini wapo ambao anayafanyia kazi na kurekebisha accordingly. Big up sana madam. Wasomaji wenzangu, penye ukweli tuwe tunasupport lakini kuna wengine kazi yao ni kuponda tu wee mtu gani lakini jamani, Shitwan Urajim!

    ReplyDelete
  8. baada ya diamond kukutema mfuate kingwendu

    ReplyDelete

Top Post Ad