Aunty Ezekiel: Sinta Mzika Wema, Familia ya Wema Yacharuka yasema Heri Kajala Kuliko Aunty

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

‘Nikifa usije kunizika, ukifa sitakuzika’! Ni maneno makali sana kuyatamka kiasi kwamba, enzi za wahenga ilipotokea ndugu, marafiki au majirani wakaapishana kwa maneno hayo, walitafutwa wazee wenye hekima ili kuondoa laana hiyo.

Sasa, hivi karibuni, baada ya kuvunjika kwa urafiki wa ‘kupika na kupakua’ kati ya mashostito wawili walio katika tasnia ya Bongo Movies, Aunt Ezekiel Grayson na Wema Isaac Sepetu maneno hayo yametumika pasipo sababu, Ijumaa Wikienda lina kila kitu!

AUNT BILA KUUMA MANENO

Juzi, Aunt ameibuka na kutoa kauli kali bila kuuma maneno kwamba, Wema akitangulia kuaga dunia, yeye hatakwenda kumzika kwa maana ya kuuaga mwili wake sanjari na kuomboleza.

KIASA CHA KAULI

Kauli hiyo ya Aunt imekuja siku chache baada ya Wema naye kudaiwa kutoa kauli kama hiyo akisema kwamba, kutokana na urafiki wake na Aunt kufa na kuwa maadui, basi hata akifa, Aunt asiende kumzika.

 MSIKIE AUNT ‘LAIVU’

Ijumaa wikienda: Aunt pole kwa kulea mimba! Nina machache sana. Wema amedaiwa kuanika hatima ya ugomvi wenu kwamba, hali ilipofikia hata akifa wewe usiende kumzika. Wewe unasemaje?

Aunt: Kwanza nashangaa taarifa za kwamba nina ugomvi na Wema maana hata hao ndugu zake nimesikia wanaongea mambo kibao.

“Ila mimi sioni kama kuweka picha ya tangazo la shoo ya Zari (Zarinah Hassan) kwenye peji yangu ya Instagram ni kosa. Kwa hiyo kama yeye hataki kuzikwa na mimi, hata mimi nasema sitamzika Wema.

 AANZA KUFUNGUKA

”Halafu sidhani kama kuna mtu anaweza kunipangia kitu kwenye peji yangu mwenyewe ambayo nina uamuzi wa kufanya chochote ninachojisikia.

 ILIKUWA UTANI, IYOBO ATAJWA

“Mimi sidhani kama hapo kuna ugomvi, maana nilichoandika na kuweka siku hiyo ilikuwa ni utani lakini hata kama yeye na ndugu zake walichukulia ‘siriasi’ basi bado walitakiwa kutambua kuwa, mchumba wangu Iyobo (Moses) ni mfanyakazi halali wa kundi la muziki la Diamond (Nasibu Abdul), hivyo nilikuwa na haki ya kumsapoti kwa asilimia zote maana fedha anazopata kupitia huko ndizo zinazonifanya mimi na familia yangu niishi,” alisema Aunt.

 FAMILIA YAWEKA KIKAO

Kufuatia vuguvugu hilo kushika kasi, hivi karibuni familia ya  Wema inadaiwa kuweka kikao na kusema kwamba walimuonya ndugu yao huyo siku nyingi kwa kumwambia kuwa, urafiki wake na Aunt ni sawa na ‘spea’ za ki-China kwani waliamini hautadumu kwa sababu ni unafiki tu bora hata alivyokuwa na Kajala Masanja.

Chanzo makini kutoka katika familia ya Wema kimelipenyezea ubuyu Ijumaa Wikienda ambapo kilitiririka:

“Mama Wema kama kawaida yake, alifikia hatua ya kusema kwa sasa hataki tena kumwona mwanaye akirudia urafiki wake na Aunt kwa sababu ni mnafiki.

 MAAZIMIO YA KIKAO YAFIKA KWA WEMA

“Maneno hayo ya mama na ndugu wengine, yalifikishwa kwa Wema, akawaelewa na kusema hana haja tena ya kuwa karibu na Aunt hata itokee nini maana hakuna anachomsaidia.”

 AUNT TENA, AMWANIKA WEMA SASA

Aunt alipoambiwa kuhusu maazimio ya kikao cha familia ya Wema na jinsi staa huyo alivyoyapokea, alisema:

 “Kama familia yake wamefikia hatua ya kuingilia hili, mimi nafikiri sina tatizo maana nina maisha yangu na yeye (Wema) ana maisha yake. Ila tu kama ni ishu ya wazazi, naomba wajue pia mimi sijajizaa wala sijazaliwa na miti, nina ndugu tena wanajitambua kwa kila hali.

“Nikiangalia sababu za ugomvi ni za kibinafsi sana hata hazifai kuingiliwa na mtu, maana haiwezekani kwenye maisha haya eti Wema akinuniana na mtu basi na mimi nimnunie, sijaumbwa hivyo wala sina unafiki huo.

“Kama staili ya maisha ikiwa kila atakayekwazana naye na mimi nimchukie siku wanapoelewana mimi si nitaonekana sifai kote? Wao wafahamu kuwa mimi najitambua wala si wa kuburuzwa hivyo.

“Kama wanasema hawawezi kushiriki lolote kwangu hata mimi sina sababu ya kujipendekeza kwao.

 WEMA AZIDI KUCHAMBULIWA

“Hakuna kitu kibaya katika maisha kama kuwa na rafiki ambaye siku zote yeye akikosana na mtu basi na wewe ukosane naye. Mbona mimi maadui zangu yeye ni marafiki zake na wala sijawahi kununa. Iweje sisi tukorofishane na watu yeye aongee nao ila yeye akikorofishana na watu basi hataki kabisa hata kutuona nao?”

 WEMA NAYE ATEMA NENO

Baada ya Ijumaa Wikienda kupata fukunyuku hizo lilimsaka Wema kwa maana ya kujiridhisha na kinachodaiwa kusemwa na yeye na familia yake, mambo yalikuwa hivi:

“Yaani hata sitamani kusikia jina la Aunt maana alichokifanya ni bora hata ya Kajala ambaye ishu yake ni ya moja kwa moja. Nashindwa kuliweka wazi sana lakini familia yangu haitaki hata kumsikia kwa jinsi ilivyochukizwa naye.

“Sifikirii kama kuna siku nitakuja kukaa naye tena au kuongea chochote mbele yake maana alichokifanya si cha kunifanyia mimi tuliyeshibana kama mapacha.”

Aunt  ‘mama kijacho’ na Wema walikuwa marafiki walioshibana kabla ya kutofautiana baada ya Aunt kutoa sapoti kwa mpenzi wa Diamond, Zari kwenye shoo yake ya Zari All White Party kwa kuposti picha kwenye mtandao iliyoonesha kupigia debe shughuli hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Mlimani City hivi karibuni jambo lililomkera Wema akiamini Aunt  ni mnafiki, yuko kwake na kwa mahasimu wake hao.
Chanzo:Global publishers
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

18 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wemaaaa, Madaaaam

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wema anazidi kuyoyoma vibaya. Kitendo cha Domo ku move on kinamchanganya kwa kiasi kikubwa mno. Kitendo cha Zari na Domo kuwa pamoja na kitumbo cha Zari kinamsugua ubongo hasa akizingatia swala la pengine ana ugumba. Kitendo cha Antie kuzaa na moja ya mastaff wa Domo kinamkosesha amani kwani anahisi kwa namna moja au nyingine Zari na Antie wata meet na kuwa close. Kitendo cha Kajala kuwa kwenye baby shower ya Antie kinazidi kumnyima usingizi. Tatizo Wema hakubali au hawezi kuishi bila mashindano. Sasa kwani familia yake ikimchukia Antie ndio itakuwaje?? Who do they think they are?? Wema is and will remain beyond repair.....Too late...

      Delete
  2. WEMA KUMBE UNAAKILI MBOVU KIASI HICHO, EMBU BADILIKA UPASWI KUWA HIVYO HAKUNA MTUMWA WAKO, KILA UNALOTAKA WW NDO LIWE HATA HAYA HUNA!!!

    ReplyDelete
  3. mmmhhh kama hali ni iyo petiti yupo mashakani! Aunty she is right tho! ila nawe wema kwani lazima uwege na mashoga una madada watatu mungu akuwekee hao wanatosha kuwa shoga zako kabisa tena punguza na awo madada wa mjini mana kila mtu dada ako!!

    ReplyDelete
  4. Wema is hurting herself for nothing. ....she's nt tha first lady kuuachwa ivo awe na hasira na kila mtu....by now she should focus ahead .....by because she can't handle tha situation of his ex ...tht y she's creating enemity with her friends ......

    ReplyDelete
  5. SAFI SANA AUNT HIVYO NDO INAVYOTAKIWA KUWA NA MSIMAMO NA SIO KUPELEKESHWA, NIMEKUPENDAJE GHAFLA MMWAAAAAAAAAAAAAAAA

    ReplyDelete
  6. Yani Wema aunt ni anaakili mana hata majibu yake ni yameenda shule... Yeye pia anafamilia yake na hao familia yako Wema ni wanafki kwahiyo since Uko na aunt walikuwa wanamsemgenya ama sasa iweje waseme tangu kipindi hiko tunasema aunt sio mzuri kwa Wema. Wewe mdada utagombana na kila mtu ktk dunia hii usitake watu wakufatilie wewe mana nao ni watu wazima na maisha yao huwapi kula wewe. Nimempenda aunt anajitambua

    ReplyDelete
  7. AUNTY UPO CORRECT WE UMEMSUPPORT MMEO SASA TATIZO LIPO WAP! JALI MAISHA YAKO MENGNE YATAKUPA STRESS BURE USHNDWE KUJIFUNGUA VZURI! MUNGU AKUJALIE UJIFUNGUE SALAMA MAMA MTARAJIWA!

    ReplyDelete
  8. Werawera Aunty,
    una akili sana.

    ReplyDelete
  9. Huyo wema ana wazimu anataka adui zake wawe adui wa rafiki zake,kwani ye ni nani?anataka kujifanya mungu mtu,ukigombana na mtu gombana naye wewe usitake na watu wengine wagombane nao kisa wana urafiki na wewe hiyo ni roho ya kishetani

    ReplyDelete
  10. Tatizo hapo ni dogo sana, tena saana, na mwenye makosa ni aunt Ezekiel. sababu kiekweli nikwamba aunt anategemea kipato cha mchumba wake Mose kama alivyosema mwenyewe hilo lipo wazi na kila mtu analielewa. Ila aunt akumbuke kwamba yeye ni rafiki wema ambae anatofauti na bosi wake Mose. Hatuwezi kujua pengine mose alimwambia aunt apige promo coz kuna alichoahidiwa na bosi wake, sasa alichotakiwa aunt kufanya ni kumuambia wema kwamba mchumba wangu ameniambia nipige promo ili wapate hela nyingi na mgao in one way or another uwemkubwa ndani ya wasafi family, u knw wat am saying huh.... sasa ilikuwa ni aunt kumwambia wema kwamba nafanya hivi coz of mchumba wake amemuagiza kufanya hivyo, au anapiga promo ili kumsaidia mchumba wake kazini na vitu kama hivyo, si unaona so hio iko wazi na inaeleweka. Sasa kama wema angekataa aunt asipige promo hapo sasa wema tungemuona mchawi na hapendi maendeleo ya wenzake, sababu kazi ya iyobo ndio inayomuweka aunt na familia yake mjini. Hapo kusingekuwa na ugomvi kabisa, aunt kama kweli ni best friend wa wema angepaswa kufanya hivyo. Best friend wako inapaswa akusapoti kwenye shida na raha, so wema asingekuwa na budi ila kumsaport best wake tu. Sasa hayo mambo ya siri aliyoyafanya aunt ni unafki na mfyangunungu. Waswahili wanasema motto mbwa, amejitoa kama mbaya ni iwe mbaya. Sababu mie nimeshaona mara nyingi sana mose na aunt na wema wakiwa pamoja wakipiga story, so nikitu ambacho kilikuwa wazi na wema there was nothing she could do about that, and she was ok with that, sasa leo aunt anakumbatiana na mabusu na kajala ni wazi kwamba anataka kumuumiza wema yani ni mswahili mswahili Fulani hivi, mbona kabla hajakorofishana na wema hatukuona hayo mabusu... She is just a colorless Devil. Wema na wewe usilazimishe watu wa gombane na watu ambao wewe uwapendi, hayakuhusu, wacha watu wafanye yao kwa maisha yao. Na ukome kukumbatiana na moto, unaona umekulipukia.

    ReplyDelete
    Replies
    1. hivi wewe ni mwanaume au mwanamke? umeongea nini hapa? tnarudi kulekule, aunt is a born free creature, hebu rudi usome upya ndo u comment. amwombe wema ruhusa kupiga promo kumsapoti mzazi mwenzie? kwani wema ndo nani? halafu alifanyaje siri kama alitumia social media kupiga hiyo promo? we nawewe umechemka. wema is a good girl ila kwenye urafiki dizaini anpenda ksujudiwa, tukiachana na hilo, uko poa sana. ajifunze

      Delete
  11. WE MDAU HAPO JUU5:2PM AMWAMBIE WEMA KWAKUWA WEMA NI NANI HASA?? KILA ATAKACHOTAKA KUFANYA MPAKA AAMBIWE?? HAKUNA MTUMWA WAKE, ANTI UMEFANYA LA MAANA HUYO SIO RAFIKI KABISA , YY WEMA KILA ATAKALO TAKA KUFANYA ALIKUWA NAMWAMBIA ANTII MPAKA NAYE AAMBIWE?? UNAJUA WEMA ANAPENDA SANA KUWA ANAWAPRLEKESHA MASHOGA ZAKE, SASA KAKUTA ANTI HAYUPO HIVYO NDO ANAMUONA MBAYA OVYOOOO, SAFI SANA ANTIIII MMWAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA

    ReplyDelete
  12. Wema elewana tu na watu lakini sio ushoga kama unavyofanya, wenzio mbona wao tu ndo wanahamia kwako hivi hujiulizi???? Yaani unawafanya wakujue maisha yako kiundani mkikorofishana wanaenda kukutangazia mambo yako yooooote nje.

    Hivi kwa mfano yule msichana alozaa na Iyobo afanye sherehe ya aina yoyote ile halafu Wema aende kwenye sherehe hiyo au aishabikie ki aina bila kumwambia Aunty - je Aunty angejisikiaje hapo??

    Mkuki mtamu kwa nguruwe kwa binadamu mchungu. Mie siwaelewi baadhi ya watu yaani hawaishi kumsakama wema as if watu woooooote ni watakatifu isipokuwa yeye tu!!! Hata kama NYANI HAONI KUNDULE but this is too much now hebu mwachani wema aishi maisha yake jamani. Kila afanyalo baya kwa walimwengu kwani MNATAKAJE SASAAA??????

    ReplyDelete
  13. Kwahiyo wewe hapo juu unasapot ugomvi wao?! Rafiki wa kweli angewapatanisha af aunt amesema ilikuwa utani,af kwan wema hajui kuwa aunt na mose ni wachumba na mose ni mfanyakaz wa wasafi? Atashindwaje kumsapot mchmba wake kisa wema,kwan wema ndo anampa kula mjini? Af hata ndugu za wema na wema woote akili moja,.. Tena wao ndo wanafik cz walikuw wanamchukia ht kabla ya tukio hilo. Wema kazi unayo mjini hapa utakosana na kila mtu

    ReplyDelete
  14. I doubt this was planned. Na kwavile alishahaidiwa kitu akaamua arushe ile caption, na walijua kwa kufanya vile watamuumiza wema na kwavile wema don't take no shit urafiki WA wema na aunty utakwisha.kweli see aunty diamond anafanya shoo ngapi mbona huzitangazi? Ile ua zenji mbona hukutangaza? I na he uliporusha hiyo caption ya party uliweza pata watu wangapi wakanunua tiketi? Be real, aunty alijua kwa kufanya vile lazima itamuumiza wema but she didn't care, ok endelea kumsupport mumeo kwa kuendelea kutangaza shoo za diamond. And leave mtoto WA watu wema alone. Fanya promo za diamond,good luck

    ReplyDelete
  15. Yani wewe uliyeandika Hiyo barua hapo juu ni mburula kama Wema mwenye

    ReplyDelete
  16. Mwenye akili ni Esma mbona hamsapoti mme wake ina maana hahampendi Petit???tukjbaline upange wa Diamond wana nguvu na ubnafsi

    ReplyDelete

Top Post Ad