Naibu Waziri wa Kazi na Ajira , Dk. Makongoro Mahanga Atangaza Kuihama CCM......Asema Atahamia CHADEMA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Naibu Waziri wa Kazi na Ajira na Mbunge wa Segerea anayemaliza muda wake,Mh. Dkt. Makongoro Mahanga, ametangaza kuihama CCM na  kuhamia  CHADEMA kutokana na kutokuwepo Demokrasia ya Kweli ndani ya CCM.

Dr. Mahanga ambaye ni Mbunge anayemaliza muda wake  kwenye Jimbo la Segerea  kwa  tiketi  ya  CCM  ametangaZA azma hiyo leo mchana baada ya  rufaa yake ya kupinga ushindi wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kipawa mama Kivela kutupiliwa mbali na Ofisi ya CCM mkoa wa Ilala.

Duru za Kisiasa zinasema kilichomponza Dr. Mahanga ni kitendo chake cha yeye kuhusika katika mpango wa kumnadi Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa kwenye nafasi ya Urais wa CCM, ambaye kwa  sasa ametangaza kugombea urais kupitia Chadema.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nenda mwana kwenda wameondoka wangapi bana, msituchoshe na tamaa zenu za madaraka, nendeni kwa hao wanafiki wanaopokea mafisadi, wapo 'kibiashara' zaidi...

    ReplyDelete
  2. Hivi Makongoro huyu ndie yule alowaambia wapiga kura wa Ukonga kwamba, 'kwanza nyinyi hamkunichagua, ni pesa yangu ndio ilo'nichagua' , wakapania kumbwaga akakimbilia Segerea. Segerea nako wamembwaga kutokana na maneno yake machafu, bora aende kwa hao 'zoa-zoa' kama gari la taka.

    ReplyDelete

Top Post Ad