Salam Jabir Nae Aibuka Kwenye Malumbano ya Video Mpya ya Ali Kiba Baada ya Baadhi Kuiponda...Asema Haya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mtangazaji wa kipindi cha Mkasi ambacho kinarushwa kupitia ting'a namba moja kwa vijana (EATV) Salama Jabir amefunguka na kuwataka watanzania kuthamini na kuheshimu watu ambao wanajituma kufanya mambo katika kazi zao.

Salama amesema kuwa kazi ya msanii siku zote ni sanaa ambayo unaweza kuipenda au kutoipenda.
Salama Jabir amesema hayo kupitia Account yake ya Twitter kufuatia baadhi ya maoni ya mashabiki ambao wamekuwa wakiwaponda wasanii wa bongo pindi wanapokuwa wanatoa kazi zao hususani video huku mashabiki wengine wakienda mbali na kuponda au kuzungumzia jambo kama wao wana maarifa ya jambo hilo.

"Kazi ya msanii ni Sanaa... Usingiingilie!! ni aidha utaipenda au hutaipenda simple!! Kama rahisi fanya na wewe tuone Respect kwa wanaojituma" Amesema Salama

Imekuwa ni kawaida kwa mashabiki kuponda kazi za wasanii na kuwatusi kupitia mitandao yao ya kijamii jambo ambalo linakuwa linakatisha tamaa baadhi ya wasanii na kuwaumiza kwani maneno ambayo mashabiki huwa wanatumia ni makali na ya kukatisha tamaa.

Hali hii mara nyingi imekuwa ikisababishwa na makundi ya mashabiki maarufu kama Team, kuna watu wanaweza kuponda jambo ili mradi tu kwa sababu yeye si shabiki wa msanii fulani na wapo wengine wanafanya hivyo kwa lengo ya kukomesha, huku wengine wakitaka wasanii waendelee kuleta video za aina fulani pekee na ukifanya vinginevyo wanaona umekosea kwa sababu ndicho kitu walichozoea kifupi hawataki kukutana na kitu cha iana mpya.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

14 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ila ukweli ile video ni mbaya, ingawa kiba kajitahidi ila huwa hakuna hualisia kbss Kati ya analoimba na linaloonekana

    ReplyDelete
  2. Watanzania, tuipende nchi yetu, tuwapende wasanii wetu, na tuwaunge mkono kwa kile wanachokifanya ili sanaa ya watanzania ijulikane kimataifa. msanii atakapokwenda nje kutangaza sanaa ya tanzania ni ajira pia kwa crue atakayoambata nayo. kwa nini tuwe na msanii mmoja tu kimataifa? kwa nini muwape ajira wageni wakati vijana wa kitanzania wapo tele mitaani hawana ajira? kuna ubaya gani katika video ya kiba lupela? acheni utumwa.

    ReplyDelete
  3. wewe unaesema mbaya fanya yako tuione. ujinga tuu

    ReplyDelete
  4. Kama mbaya mbaya na kama nzuri nzuri tu. ..duniani kote kama msanii anafanya kazi sio nzuri husemwa mana wasanii hufanya kazi kwa fun wao na kama fun hawakuipenda basi atatengeneza kazi nzuri zaidi ..

    ReplyDelete
  5. Kama mbaya mbaya na kama nzuri nzuri tu. ..duniani kote kama msanii anafanya kazi sio nzuri husemwa mana wasanii hufanya kazi kwa fun wao na kama fun hawakuipenda basi atatengeneza kazi nzuri zaidi ..

    ReplyDelete
  6. Jamani ni mbaya kwenu wengine tumeipendaaaaaaaaa.

    ReplyDelete
  7. Uhalisia wa video na vitendo maneno are different just tuwe honest ili pale penye kosa mtu ajirekebishe usikubali kusifiwa kwa shadow angle

    ReplyDelete
  8. ni nzuri sana kabadilisha yalee ya magorofa na mapenzi ya kila cku.

    ReplyDelete
  9. NYIMBO YA KIUTU UZIMA, ILOKWENDA SULE, HONGERA KIBA.

    ReplyDelete
  10. watanzania wengi wana wehu wanaosema mbaya angalia hata walivo utacheka ukicheki picha zao walivopiga majanga ila kukosoa wenzao wanakuwa wa kwanza na wengi wenye tabia za kukosoa watu ukiwafatilia wanalala kwa dada zao tena jikoni

    ReplyDelete
  11. Huyo Salama mbona kwenye bongo star search ndio anaongoza kwa kuponda sanaa za watu

    ReplyDelete
  12. nyimbo iko poa anaesema iko tofauti sbb hajui sanaa ni nini sanaa ni ubunifu na kiba amebuni kitu rudini shule mkasome Kiswahili mtaelewa zaid kiba upo juu wewe ni mkali msanii unaejua kubuni na kuleta vitu tofauti hio ndio sanaa poleni wenye kukosoa watu hali ya kua nyinyi wenyewe hamjijui mpo tu

    ReplyDelete
  13. Ukweli usemwe tu

    ReplyDelete

Top Post Ad