Kichwa Cha Binadamu Kuanza Kupandikizwa kwa Operation Kwenye Mwili wa Mtu Mwingine

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mtaalam wa upasuaji wa mfumo wa neva (neurosurgeon) Sergio Canavero kutoka nchini Italia, anakusudia kufanya jaribio la kwanza la kupandikiza kichwa cha binadamu kwenye mwili wa binadamu mwingine, ifikapo mwakani.

Wataalam wengi wa upasuaji wanafikiria wazo hilo ni la kiuwendawazimu, lakini sio kwa mtaalamu huyo, kwani anasema bado anapanga kujaribu pandikizo la kwanza la kichwa kwa binaadamu. (Head Transplant)

Dk. Canavero ambaye mpaka sasa ameshapata mtu wa kujitolea kufanya zoezi hilo, kijana mwenye asili ya Urusi ambaye ni mtaalam wa software Valery Spiridonov, ambaye ana tatizo la kupoteza nguvu kwa misuli yake ya mwili.

Dk. Canavero amesema mafanikio yake yameonesha kuwa mpango wake wa kupandikiza kichwa cha binadamu kwa mwili wa mtoaji (donor) bado upo, na ataanza mpango huo mwishoni mwa mwaka 2017 na unaweza kuwa njia ya kutibu waliopooza mwili.

“Ningesema tuna takwimu nyingi zinaendelea, ni muhimu kwa watu kuacha kufikiria jambo hili sio rahisi, hii inawezekana kabisa na tunaendelea kulifanyia kazi”, alisikika Dk, Canavero akimwambia mwanasayansi mchanga.

Timu iliyo nyuma ya kazi hiyo ilipost video ikimuonesha nyani ambaye alifanyiwa upandikizwaji huo, na kufanikiwa kutembea baada ya uti wa mgongo kutenganishwa na kuunganishwa tena'
Upandikizwaji wa kichwa kwa nyani ulifanywa katika chuo cha Harbin nchini China ( Harbin Medical University) na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa, bila kuwa na muathiriko wowote katika uti wa mgongo, lakini aliuawa baada ya masaa 20 baadaye, kutokana na sheria za kazi.

Dk. Canavero amesema atahitaji pesa nyingi ili kuwalipa timu ya upasuaji, kwa mtu wa kwanza ambaye ni raia wa Urusi, hivyo amemuomba mwanasayansi tajiri zaidi Mark Zuckerberg, kufadhili upasuaji huo.
Picha ya Nyani aliyepandikizwa kichwa.
Kijana Valery Spiridonov aliyejitolea kufanyiwa upandikizwaji huo wa kwanza, ambaye mwili wake una tatizo la misuli.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Daaah watu wenye akili zao tz tuna wataalam wa nn au majipu ndo yamejaa tz na wataalam wa wezi wa wake na waume za watu...

    ReplyDelete
  2. Mmh! Hapo bado sijaelewa wajameni. Huyo dogo amekubali kupandikizwa kichwa, sasa hicho kichwa anachopandikizwa kinatoka wapi??? Au ni hicho hicho chake kinakatwa wanarekebisha misuli kisha kinapandikizwa tena?? Ikiwa hicho kichwa kitakuwa 'kipya', je atakuwa ni yeye yule yule na akili zake zile zile?? Nina maswali mengi kuliko majibu.....YETU MACHO. sisi tunaruka na ungo, hawatuwezi

    ReplyDelete
  3. Ano 4:42
    Huyo raia kichwa chake kitapandikizwa pengine,kajitolea maana mwili wake hauna nguvu vizuri.

    ReplyDelete
  4. wewe mtu mweusi anaweza kutomba tu akili zipo kwenye pumbu., waachieni wazungu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pia tunao uwezo wa kugeuza 'ungo' kuwa 'jet' hahahahah

      Delete

Top Post Ad