Alichokizungumza Tundu Lissu Kuhusu Mbunge wa Kilombero Kufungwa Miezi Sita

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

HATUA ya Mahakama ya Wilaya ya Kilombero, Morogoro kumfunga Peter Lijualikali, Mbunge wa Jimbo la Kilombero miezi sita jela, inatokana na visa vya kisiasa

Ni kauli ya Tundu Lissu, Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) leo mbele ya waandishi wa habari aliokutana nao kwenye Makao Makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki amesema kuwa, vita kati ya upinzani na Chama Cha Mapinduzi (CCM) vimesababisha Lijuakali (Chadema) kupata hukumu hiyo ya kisiasa.

Mbele ya waandishi wa habari Lissu amesema kuwa, “hiyo ni hukumu ya kisiasa” na kwamba, Jeshi la Polisi nalo limeingizwa kwenye vita hivyo.

Lissu amesema, chanzo cha hukumu hiyo kinatokana na mgogoro wa uongozi ndani ya Halmashauri ya Kiliombero ambapo Chadema na washirika wake wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) walishinda madiwani wengi.

Hivyo, kwa mujibu wa Lissu, Halmashauri ya Kilombero ilipaswa kuongozwa na mwenyekiti anayetoka na Ukawa na awe Chadema.

“Ili hilo lisiwezekane, na ili CCM wachukue Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero licha ya kushidwa kwenye udiwani, ilibidi wamfanyie Lijualikali mambo ya ajabu,” amesema Lissu.

Lijualikali (30) amehukumiwa jana kwa kosa la kufanya fujo na kusababisha taharuki. Huku Stephano Mgata (35), Dereva wake ambaye ni mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo akifungwa kifungo cha miezi sita nje.

“Kifungo cha Mh. Lijualikali ni adhabu ya kisiasa. Mh Lijualikali ni mfugwa wa kisiasa. Amefugwa kwa sababu ya siasa.

“Adhabu ya kisisa ni vita ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) dhidi ya Chadema na wanatumia Jeshi la Polisi, wanatumia mahakama na kwingineko. Vita hii hii wanawatumia akina Lipumba (Profesa Ibrahim Lipumba,” amesema Lissu na kuongeza;

“Kwingine wamemweka Lema (Godbless Lema, Mbunge wa Arusha Mjini) mahabusu kwa miezi mitatu. Hakuna jinai yoyote. Tuliwashinda kwenye uchaguzi.

“Sasa baada ya uchaguzi walimfungulia Lijualikali kesi ya kupinga matokeo mahakama kuu, tukawapiga chini. Wamefungua rufaa na tunawatandika.”

Mwanasheria huyo amesema kuwa, nchi hii ina wafungwa wa kisiasa na kwamba, pamoja na CCM kudhani kwamba, kumfungulia kesi Lijuakali kutawapa afueni. Wasahau.

“Tuna wafungwa wa kisiasa nchi hii. Wale wanaofikiria kwamba kumfunga Lijualikali CCM itapendwa na wananchi wa kilombelo wasahau hilo.

“Huwezi kuwatesa wananchi, ukatesa viongozi waliowachagua kwa mapenzi yao halafu ukategemea wakupende. Wasahau,” amesema Lissu.

Aidha, Lissu ametoa ufafanuzi kuwa Ibara ya 67 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inamlinda Lijualikali hivyo hawezi kupoteza ubunge wake kutokana na hukumu hiyo.

Amesema Chadema hakijaridhika na hukumu hiyo, hivyo kwa sasa wanaandaa utaratibu wa kisheria ili kukata rufaa kuipinga ambapo hatua hiyo inaweza kuchukua siku mbili kukamilika.

Timothy Lyon, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo alisema, amemhukumu Lijualikali baada ya kumtia hatiani kwa kosa yeye na dereva wake na kwa kuwa, mbunge huyo alipatikana na hatia katika kesi tatu huko nyuma na kuhukumiwa kulipa faini hivyo alistahili kutumikia adhabu hiyo.

Kesi zilkizotajwa na Lyon zinazomuhusu Lijualikali ni namba 338, namba 220 na namba 340 zote za mwaka 2014.

Katika kesi hiyo, Dotto Ngimbwa, Inspekta wa Polisi aliiambia mahakama kuwa, Lijuakali akiwa mshtakiwa namba moja pamoja na Mgata walitenda kosa hilo Machi Mosi mwaka 2016 eneo la Kibaoni katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kialombero na kwamba, walifanya fujo kinyume cha sheria.

Alisema tukio hilo lilitokea Machi Mosi mwaka huo saa 4 asubuhi ambapo washtakiwa walikana mashtaka lakini upande wa mashtaka ukathibitisha bila kuacha shaka kwamba, walitenda kosa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Pamoja na hoja zako Mh, Tundu Lissu, bado ukubali kuwa wale mnaowapendekeza kuwa wagomba wnu katika nyazifa mbalimbali lazima wawe na kasoro za kimaadili kana kwamba chama chako hakiitaji watu wnye kutumia akili nakuwa na ngozi ngumu ya kisiasa. Sina haja a kuwataja wabung na hata madiwani wenye sifa nilizozitaja,ikumbukwe kwa sasa Tanzania ni huru atutafuti uhuru hao watu wa namna hiyo walihitajika miaka ya 50. Ili umoja wenu uweze kuwa wa mafanikio usitafute huruma kwa wananchi kitu ambacho nakiona ni ghiliba kwa wananchi, hawa wanafanya makosa wazi tena kwa kujua wanafanya makosa na wanajua kitakachowatokea. Mpaka kufikia level ya kuwa mbunge ni kwamba bila kupepesa macho mtu huyo ni mweledi , msikivu, anatumia akili badala ya nguvu, anaheshimu wenzake anaepuka lugha za kuudhi na kutanguliza mbele sheria na kanuni zinazoongoza taifa, hivi wabunge hawa wa UKAWA, wanalifahamu hili? kamahawalifahamu basi uenda wataishia ndani kwelikweli, wafuate sheria na culture ya taifa letu, hayo wanayoyafanya tumechoka nayo tunayasikia kwa wenzetu na atushangai kwni historia haipo mbali na wao. Acheni kutengeneza scenario katika siasa kuweni realistic na wananchi watawaelewa, Rais ni mmoja ni JPM na ni awamu ya tano.

    ReplyDelete
  2. SWALI KWA CHADEMA,HIVI KWANI HUYU LISSU HAWEZI KUSIMAMA KUGOMBEA URAIS 2020?

    ReplyDelete
  3. Lissu zungumza kisheria sio kisiasa, sisi tunaoishi huku Kilombero tunajua mikiki isiyo na maana ya huyo Mbunge, kimsingi kateni rufaa kama hamjaridhika na hukumu na adhabu na sio kusingizia vyombo vingine, pia ni busara kumshauri huyo kijana aache utoto yeye ni mbuunge sasa na ajue kuwa wananchi tuliompa dhamana ya kutuwakilisha tunakwazika anapofanya mambo ambayo hatujamtuma kuyafanya.

    ReplyDelete
  4. Lissu, Ama kweli!! Leo unaweza kuzungumzia Chombo cha Kutoa Haki Umekidhalilisha kwamba hiki ni Sawa na tekelezi la sera na miundo ya chama unachokituhumu .. Kumbuka kesi zako tunazo na unahitajika kizijibu na pindi ukiiendelea na tabia yako hii na dharau zako hizi jua unapokwenda ni kule kule kwa watovu wa nidhamu na wewe unajidhihirisha kuwa ni lingi lida kama mtowe. Badilika na ujitambue wewe liuhalisia wako.. Mkosa nidhamu...Hapa Kazi tu

    ReplyDelete
  5. Lissu, Ama kweli!! Leo unaweza kuzungumzia Chombo cha Kutoa Haki Umekidhalilisha kwamba hiki ni Sawa na tekelezi la sera na miundo ya chama unachokituhumu .. Kumbuka kesi zako tunazo na unahitajika kizijibu na pindi ukiiendelea na tabia yako hii na dharau zako hizi jua unapokwenda ni kule kule kwa watovu wa nidhamu na wewe unajidhihirisha kuwa ni lingi lida kama mtowe. Badilika na ujitambue wewe liuhalisia wako.. Mkosa nidhamu...Hapa Kazi tu

    ReplyDelete
  6. Lissu mtundu... unaijua Mahakama na Madaraka yake iliyopewa kisheria?? Mbona unakosa Maadili na Utovu wako wa Nidhamu na Heshima unaanza kukiuka mipaka!!

    ReplyDelete
  7. Lissu mtundu... unaijua Mahakama na Madaraka yake iliyopewa kisheria?? Mbona unakosa Maadili na Utovu wako wa Nidhamu na Heshima unaanza kukiuka mipaka!!

    ReplyDelete
  8. wEWE NA yEYE NI WAKUSAIDIA UPELELEZI WA BEN SANANE. MZEE FUCUS ANA USONGO NA SISI PIA. MSIPOTEZE USHAHIDI KWA KUWAACHENI NJEE. HIVI PUNDE TUTAWAHITAJI. SHERIA NI MSUMENO.. WALA HAIANGALII. MTOTO WA WATU HAPOTEZWI BURE. MLISHA TAKA KUMFANYIA HUYU MZALENDO ACT ION. MACHALE YAMCHEZA.. KWANI UONGO?

    ReplyDelete

Top Post Ad