11 Jan 2017

Mwanaume Ataka Kumlipa Mungu Pesa Ili Amsamehe Dhambi zake...Azikwa na Dola Elfu Tano

Charles Obong alitaka kumlimpa Mungu ili ampe msamaha kwa dhambi zake

Mwanamume mmoja nchini Uganda amezikwa pamoja na dola 5,700 pesa taslim, ambazo alitaka kumlimpa Mungu ili ampe msamaha kwa dhambi zake na kumuokoa kutoka kwa moto wa ahera.

Charles Obong, mfanyakazi wa zamani wa serikali ambaye aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 52, aliomba hilo kwenye wosia wake, kwa mujibu wa familia yake.

Licha hiyo kutekelezwa, kaburi lake lilifukuliwa na pesa hizo kuondolewa kutoka wa jeneza lake, baada ya wazee wa jamii kufahamu kilichotokea, kwa mujibu wa gazeti la the Daily Monitor.

Gazeti hilo lilimnukuu askofu mmoja wa kiangilikana Joel Agel, akisema hakuna pesa zinazoweza kununu uzima wa milele na Mungu hawezia kupokea pesa kama malipo.


Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD

Share:
Weka Maoni yako Hapa

1 comment:

  1. du waafrika wana tamaa ya pesa utafikiri nini mpaka inakera, yaani watu wana tamaa ya pesa mpaka wanafukua kaburi? Kama jamaa ilikuwa ni wosia wake azikwe na pesa zake sasa kwa nini wamnyime haki yake, hivi watu hawajui maana ya wosia ni nini? Wosia hauwezi kukatishwa na mtu yeyote hata kama Mungu hawezi kupokea malipo ya pesa, mbona kuna wazungu wanazikwa na pesa zao na hamna ndugu yeyote atakayekata wosia wa mtu kwa wazungu, hiyo inaonyesha wazi waafrika wana tamaa sana ya pesa kuliko kumheshimu mtu na wosia wake sababu hiyo ni haki ya binadamu anapofariki

    ReplyDelete

Total Pageviews


Popular Posts

Matangazo

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger