• Hot Topic

  16 Apr 2017

  Breaking News..Mbunge wa Chadema Alazwa Ghafla Muhimbili..Afanyiwa Upasuaji Kuokoa Maisha Yake..!!!


  Wakuu salaam. Natumai tupo wazima. Kama inavyozunguka mitandaoni kuhusu kulazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa Mhe. John Heche, taarifa hiyo ni ya kweli. 

  Mhe. Heche alifika Hospitali ya Taifa Muhimbili siku ya Jumanne wiki hii kwa uchunguzi wa afya yake, baada ya uchunguzi wa awali alishauriana na daktari wake na kukubaliana angerejea Hospitali baada ya wiki mbili kwa matibabu rasmi.

  Hata hivyo jana usiku 
  Mhe. Heche alipata maumivu makali ya ghafla tumboni na leo asubuhi alikimbizwa Hospitali Muhimbili na kufanyiwa upasuaji (specialised surgery).

  Upasuaji umeenda vizuri na hali yake inaendelea vema sana. Mwenyekiti wa Taifa Mhe. Freeman Mbowe amemtembelea kumjulia hali. 

  Salum Mwalim
  Naibu Katibu Mkuu
  CHADEMA 
  Jumapili April 17, 2017

  No comments:

  Post a Comment


  Mapenzi

  Hot Gossip

  Siasa