HIZI Hapa Faida Za Maharage Meusi Mwilini..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Baadhi  ya watu hawapendi kutumia maharage kama mboga kutokana na kuonekana kama ni chakula cha kimaskini, lakini kiafya maharage ni miongoni mwa mboga zenye faida kubwa mwilini na hutoa ahueni kubwa kwa watu wenye matatizo mbalimbali ya kiafya kama tutakavyoona leo katika makala haya;

Kwa mujibu wa utafiti mbalimbali, maharage, hasa meusi ni chanzo kizuri cha kirutubisho aina ya faiba kinachoshusha kiwango cha kolestro mwilini, vilevile kiwango cha faiba kilichomo kwenye maharage meusi, huweza kudhibiti kiwango cha sukari kisipande haraka baada ya chakula, hivyo kufanya maharage kuwa lishe nzuri kwa wagonjwa wa kisukari na shinikizo la juu la damu.

Iwapo utapata mchanganyiko wa maharage meusi na ule mchele ‘mweusi’ ambao haujakobolewa na kuondolewa virutubisho vyake muhimu brown rice, basi utaweza kupata kiasi kikubwa cha protini na faiba ambacho huwezi kupata kutoka katika chakula kingine.

Aidha, utafiti wa muda mrefu uliofanywa na jarida moja lijulikanalo kama Journal of Agriculture and Food Chemistry, unaonesha kuwa mbali ya maharage kuwa na kiwango kikubwa cha faiba, pia maharage yana virutubisho vingine vinavyojulikana kama Anthocyanins ambavyo hutoa kinga mwilini Antioxidant.

Kiwango cha virutubisho hivyo kilichomo kwenye maharage, kinaelezwa kuwa ni kikubwa kuliko hata kinachopatikana kwenye matunda kama zabibu ambayo inaaminika kuwa na kiwango kikubwa zaidi.

Inaelezwa pia kuwa, watafiti walipofanya tathmini ya ziada kwenye maharage, waliweza kubaini kuwa maharage yanapokuwa meusi zaidi, ndivyo ambavyo kiwango kikubwa cha kinga kinavyoweza kupatikana, yakifuatiwa na maharage ya rangi nyekundu, kahawia, njano na mwisho meupe.

Hii ina maana kwamba maharage meusi ndiyo yana virutubisho vingi zaidi kuliko maharage meupe na rangi nyingine.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad