Gossip, Politics And Love Affairs

ADC yapingana na TRA Kuvifungia Vituo vya Mafuta

Katibu Mkuu wa Chama Cha Alliance for Democratic Change (ADC) Doyo Hassan Doyo ameitaka Mamlaka ya Mapato nchini TRA kusitisha zoezi la kuvifungia vituo vya mafuta nchini kwani limewakosesha huduma watanzania wengi ambao kimsingi hawana hatia na hadha wanayoipata.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Alliance for Democratic Change (ADC) Doyo Hassan Doyo

Akizungumza Jumapili Jijini Dar es Salaam katika ofisi za chama hicho zilizopo Buguruni Rozana Katibu Mkuu huyo ameeleza kuwa ni vyema serikali ikawachukulia hatua za kisheria wamiliki wa vituo hivyo mafuta na kuruhusu huduma ziendelee kwani huduma ya mafuta imeendelea kuwa mtihani kwa wananchi wa maeneo mbalimbali hapa nchini.

Mamlaka ya Mapato nchini ipo katika oparesheni ya kuvifungia vituo vya mafuta nchini ambazo havijafunga mashine za EFD katika ‘Pump ‘ za mafuta jambo ambalo halichochei ukusanywaji wa mapato wenye ukweli wa takwimu.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu Doyo amesema ADC inakitaka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kutoingilia Mgogoro ulikuwepo Ndani ya Chama cha Wananchi CUF.

Ambapo amesema kuwa Chadema kuingilia Mgororo wa CUF kunaweza kuhatarisha amani ya nchi.

“Tumeshuhudia Migogoro mingi ya vyama vya siasa lakini hatujaona kingene kikiingilia Mgogoro wa Chama kingine”.

Hata hivyo Doyo ameitaka serikali iviache vyama vya siasa nchini vifanye shughuli zao.

ADC ipo katika maandalizi ya Maadhimisho ya kuzaliwa kwa Chama hicho ambayo yatafanyika Tarehe 22 Agosti Mwaka Huu ambapo chama hicho kitakuwa na ziara kwenye asasi za Kiraia, kuwatembea Wagonjwa, Wafungwa, Vyuo vikuu na Kutembea Nyerere Foundation ,N.K na Mwisho kuhitimisha kwenye Ofisi za chama hicho Buguruni Jijini Dar es Salaam, huku vyama mbalimbali vikialikwa.Tupe Maoni Yako
Lebel:

Post a Comment

[blogger]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget