Hamisa Mobetto Amfungulia Kesi ya Madai Diamond Platnumz

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwanamitindo Hamisa Hassan Mobetto amemfungulia kesi ya madai mzazi mwenzie, Msanii Naseeb Abdul @diamondplatnumz kwa madai ya kushindwa kumuomba radhi pamoja na kutotoa fedha za matunzo ya mtoto wao, Abdul Naseeb Juma.
.
Wito huo wa Diamond umewasilishwa na mawakili wa @hamisamobetto, Abdullah Zulu na Walter Godluck kutoka Kampuni ya Uwakili ya Century Attorneys.
.
Katika wito huo Diamond anadaiwa kumdhalilisha na kutompa matumizi ya mtoto kwa takribani miezi miwili.
.
Wakili Zulu akizungumza na Gazeti la Mwananchi, amesema mteja wao Hamisa Mobetto alimtumia Diamond notisi ya kumuomba radhi na kumtaka apeleke matunzo ya mtoto ndani ya siku saba.
.
“Baada ya kuona kimya tulipeleka kes i katika Mahakama ya Kisutu upande wa watoto (The Juvenile Court Of Dar es Salaam) na leo(Alhamisi) tumepewa barua ya wito na tayari mwanasheria wa mwanamuziki huyo ameipokea,” amesema.
.
Shauri hilo linatarajiwa kutajwa ifikapo Oktoba 30, 2017 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. sijui kama hii habari ni ya kweli au udaku tu.
    sujui ujumbe huu unaweza kukufikia wewe zari mama watano.
    mwanamke mwenye hekima hujenga nyumba yake kwa mikono yake lakini aliye mpumbavu hubomoa mwenyewe pale mawinbi mazito yanapokuja bila huruma.ukitaka kujua mke mwema utamuona hata kwa matendo tu. utakuwa mpumbavu kama utaamua kuachana na diamond na nitakuona wa ajabu kuzikiliza ya watu ukabomoa uhusiano wako na mpenzi wako.wapita njia wapo,waalikwa wapo. nitakuona waajabu ukiikimbia nyumba yako sababu ya mpita njia. mbona wewe diamond amezaa na mobeto hujashitaki lolote polisi au anajiona yeye hana makosa?naomba ujumbe huu ukufikie, kaa chini negociate na diamond sababu mobeto ni mpita njia sio mwolewaji. kosa la kutokutoa hela ya matumizi kwa miezi hiyo sio jambo la kukimbilia mahakamani kushitaki umupendaye. hii ni moja kwa moja kwamba kafanya hivyo afuruge maendeleyo yenu na kuwarudisha nyuma.ni wanawake wengi wamekimbia nyumba zao na kuja kukuta wapita njia wameshindwa , jaribu kujiuliza leo uachane na diamond halafu mpita njia kachukua nafasi yako kwa muda , kisha badaye ukarudiana naye baada mpita njia kushindwa, huoni kama utakuwa umerudi nyuma sana kimaendeleo na kizekolojia.huu ni muda wako kiwacha mbali udaku na kuangalia familia yako sio kivingine.tumia nafasi hii kushida uovu huu.mimi sio shabiki wa bongo fleva wala diamond au wewe.ila shinda hili wapita njia wapate aibu. wabaki na mafile ya mahaka mikononi.wewe ubaki ukupeta na familia mkononi.

    ReplyDelete

Top Post Ad