Waziri Kigwangalla Ajibu Hoja ya Mange Kimambi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri Kigwangalla Ajibu Hoja ya Mange Kimambi
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla amefunguka na kujibu hoja ambayo Mwanaharakati wa mambo ya siasa mtandaoni, Mange aliibua kwenye mtandao wake Instagram kudai Waziri huyo ameshiriki kuwaingiza chaka Watanzania ili watapeliwe pesa


Waziri Kigwangalla akijibu hoja hiyo amesema kwamba yeye alialikwa kama mgeni wa heshima na kuwa alikuwa hawatambui watu hao binafsi na wala biashara yao alikuwa haitambui na alipoitwa kuzindua tawi lao hapa nchini alishindwa kuwakatalia ila hana maslahi binafsi katika kampuni hiyo. 

"Nimeona nitoe ufafanuzi kwenye hili jambo. Maana kila mjadala juu ya hii kampuni ya ..... unapoibuka, jina langu linakuja, na mara nyingine picha yangu inawekwa. Ukweli ni kwamba, nilialikwa kwenye shughuli ya uzinduzi wake kama mgeni wa heshima; mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa wakati huo, Dr. Adelhelm Meru. Niliamini kwa heshima ya kuzinduliwa rasmi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, ambao ndiyo wenye dhamana ya usajili wa biashara zote nchini, ni lazima ni watu halali na bado ninaamini kama kuna shida mamlaka husika zitachunguza na kuchukua hatua stahiki na kama hakuna shida basi ni vema mamlaka husika zikatoa mwongozo utakaowaondoa hofu wananchi wenzetu wenye ‘interest’ ya kushiriki kwenye biashara hii"

"Baada ya kufika eneo la tukio, kiitifaki ikaonekana nami lazima nishiriki zoezi, nikashindwa kukataa. Nadhani inafahamika kwamba nimekuwa mstari wa mbele kuunga mkono kwa vitendo jitihada nyingi mbalimbali za wajasiriamali vijana ambao wameamua kutoka #NjeYaBox. Hata hawa nilishindwa kuwakatalia. Ukweli ni kuwa, siwajui wao binafsi ‘at personal’ level na wala biashara yao, umiliki wake na muundo wake siujui zaidi ya kuelewa kwa juu juu kuwa ni ‘network marketing’. Ifahamike hapa kuwa sina maslahi yoyote yale kwenye biashara hii na wala sikushiriki uzinduzi wake kwa malengo ya kutoa ushawishi ili watu wajiunge, na natoa rai kwamba wanaotaka kujiunga ama kuacha kujiunga wasitumie picha za ushiriki wangu siku ya uzinduzi, kwa namna yoyote ile, kujenga uhalali wa aina yoyote ile, bali watumie vipimo vyao vingine kufanya uamuzi na siyo picha zangu" alisema Kigwangalla

Mbali na hilo Waziri Kigwangalla aliwaonya watu mbalimbali na Taasisi ambazo zimekuwa zikitumia picha yake hiyo kwa lengo la kuhamasisha watu kushiriki katika biashara hiyo na kusema hatahusika na matokeo yoyote yale na kuwa akibaini kuna mtu au Taasisi inafanya hivyo atachukua hatua za kisheria.

"Sintohusika na matokeo yoyote yale, chanya ama hasi, ya ushiriki wa mtu yeyote yule ama taasisi yoyote ile, kwenye shughuli za kampuni hii. Naomba pia izingatiwe kwamba, jina langu ama picha yangu haijaruhusiwa kutumika kama bango la matangazo ya biashara ya mtu au taasisi yoyote ile, na hivyo kufanya hivyo ni kosa kisheria na ikibainika nitachukua hatua kali za kisheria" alisisitiza

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ndugu Kigwangala, umeingia kwenye siasa chafu. Umeshindwa kuwa shujaa kutokana na njaa zako. Umebabaika sana kisiasa. UnawKama ulikubali kuzindua si ulitumika tu, upo. Nyinyi wasomi wa maneno mengi, mnakurupuka sana. Hamna maadili ingawa mnapreach. Mnajidai wazalendo ni maneno matupu ingawa mnajua uzalendo ni kitu gani, na mmekaa na nchi zenye wazalendo. Kazi zenu kubwa kuhubiri na si kuidhi kizalendo ndo kitu kilichokurudisha CCM. Maslahi, ubinafsi, urahisi wa kimaisha bila jasho. Umegeuka kuwa mhubiri tu na najua unanielewa namaanisha nini. Mnatumika sana na vijizungu vijana sababu mnajua kizungu chao na wanajua udhaifu wenu wengi watanzania wadomi vijana kama wewe. Mmeshindwa kwao, mnashirikiana nao kuuhujumu uchumi wa nchi na kuwaweka watu mkenge.mnawachezea watanzania kupitia siasa na vyeo vyenu na hamna maadili. Ni aibu kujifanya wasomi wenye experience, na kuliangusha taifa letu kwa maslahi yenu ya ubinafsi. Nchi haiendelei sababu mtu kama wewe ni viboys vya wazungu. Mnaonekana wasomi lakini hamna majukuu kama waafrika. Waafrika wasomi kama nyinyi mnaishia kwenye mazingira ya siasa sababu si wabunifu wa miradi mkajiajiri na kuwaajiri vijana wenzenu. Mnabobea kwenye siasa sababu ya uhusiano na connections za wazazi wenu kisiasa. Ni nyinyi mnaozorotesha Taifa hili na muone haya. Mnajua kabisa mfanyayo. Mnajaziwa mifuko yenu kwa namna moja au nyingine. Na wengi wenu mmerudi ccm ambako mnathaminika lakini ni waongo watupu. Mmeshindwa kuwatetea watanzania, kutetea na kupigania uhuru wa mtanzania, haki na usawa kwa watanzania wote. Mnashindwa kusaidia kuulinda uchumi na mali za watanzania sababu hamna mabavu. Badala yake mnatumia siasa nyepesi kukolaborati na vibaraka majizi wa taifa na kamwe vijana kama nyinyi mtakuwa na nguvu nchini. Mtazidi kuwa vibaraka vyao. Mnajiuza na kuwauza watanzania kupitia umaskini wenu kiakili . badala ya kuungana kumsaidia raisi kikwelikweli mnaingie kwenye mikenge kukandamiza, danganya, na wizi. Mwogopeni Mungu. Na muwe na hadhi badala ya kunyonga cheap suti tu.vazi halistahili matako.Liji mtakuwa mashujaa, wakweli, wenye utu na hekima. Inachukua mtu kama Kimange mwanamke kuwaibua kila kukicha na mnafanya mambo kwa kujificha. Kati ya hao watu hawaridhiki na mienendo yenu na ndo maana Mange anazipata habari nyingi. Ujue, Watu wamechoka na wanataka mabadiliko ya kweki .wanatoka jasho ili wajikwamue nyinyi mnajipatia madlahi kwa kwenda ubia na wezi na wadanganyifu wa nchi hii ambao wanaingia kila siku kutoka nchi za nje wakijipenyesha kupitia nyinyi wajinga msio na uzalendo na busara. Mnaaibisha taifa ambalo haliendelei. Wasomi mna matatizo ya kujiamini.

    ReplyDelete
  2. Unawajua wauaji mbona umekaa kimya. Unangojea Mange akupe lako ndo ulopoke. Unamjua muuaji unakaa kimya badi nawe ni muuji pia. Acheni uhuni vijana mliopewa madaraka na kuichezea nchi na watu wake. Mmepewa dhamana msiyostahili. Mmepewa vyeo msivyostahili, wengi wenu.

    ReplyDelete

Top Post Ad