AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA JUNI 15, 2013 SAA 11:00 ASUBUHI
ONYESHO
la mwanamuziki Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ kutimiza miaka 13
katika muziki, limefana usiku wa kuamkia leo katika eneo la maegesho ya
magari kwenye ukumbi wa Nyumbani, Lounge, eneo la Kinondoni, Dar es
Salaam kwa mamia kujitokeza kiasi cha kujaza eneo hilo, hadi kupishana
ikawa taabu.
Watoto wa mjini wanasema ilikuwa funika bovu- ndiyo shoo hiyo ilikuwa nzuri mno, ya kistaarabu, yenye mashamsham ya aina yake.
|
Jide akikumbatiana na Profesa Jay |
|
Jay akipagawisha |
|
Jay akisema na nyomi |
|
Mzee Kitime akimpiga picha Komando Kalala wakati anaimba |
|
Komando Kalala na mkewe jukwaani |
|
Msanii Mango Star na nyoka |
|
Mango Star na nyoka |
Wasanii
nguli wa Hip hop waliomsindikiza Jadyee katika shoo hiyo, Mbunge wa
Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Joseph Haule na Juma Nature na
kundi lake wanaume Halisi nao walifanya mambo mazuri jukwaani kiasi cha
kuiongezea utamu shoo hiyo.
Kufika
saa 3:00 usiku tayari Machozi Band inayomilikiwa na Jide ilikuwa
jukwaani kuanza kutumbuiza kabla ya kumpisha rapa Wakazi kutoka Ukonga,
baadaye bendi ya M ikiongozwa na Grace Matata kwa shoo za utangulizi.
Saa
5:00 usiku, Jide akapanda jukwaani na kuibua shangwe nzito kutoka kwa
mamia waliokuwa wamefurika katika eneo hilo. Jaydee alianza na wimbo wa
Nilishakuwaga na Wangu, baadaye akaimba Nakuhitaji, Moto, Mambo Bado,
Yeye, Malaika, Siri Yangu, Wanock Nok kisha kumalizia na Single Boy
katika awamu ya kwanza.
Baada
ya hapo, Jide akasema ilipotimu Saa 6:00 usiku ameingia katika mwaka
mpya tangu azaliwe hivyo mashabiki wakamuimbia ‘Happy Birth Day’ kisha
akateremka kwenda kukumbatiana na mama yake mzazi, Martha Mbibo na kumpa
zawadi ya fedha zote alizokuwa ametuzwa jukwaani.
Jide
alirejea jukwaani na kuimba kwa ufupi nyimbo alizowahi kurekodi na
wasanii Man Ngwair na Langa Kileo ambao hivi sasa ni marehemu, kabla ya
kumpisha Mh. Mbunge wa Mbeya Mjini, Sugu ambaye aliimba nyimbo tatu tu,
lakini alisisimua mashabiki ile mbaya.
Sugu alianza na Hakuna Matata akimshirikisha Mkoloni, Sugu na kumalizia na Mambo ya Fedha ambao ulimrejesha jukwaani Jide.
Kutoka
hapo, ikawadia zamu ya Wanaume Halisi kutoka Temeke, wakiongoza na Juma
Kassim Kiroboto ‘Sir Nature’, ambao nao walifanya balaa vile vile na
kuurusha umati ile mbaya.
|
Msanii M2 The P akizungumza jukwaani |
|
KR Mulla |
|
Sir Nature |
|
Nature na Doro |
|
Sinta akimpiga picha Nature |
Wakati
Nature anaimba, mpenzi wake wa zamani Christine Manongi ‘Sinta’ alikuwa
bize kumpiga picha ‘mzee’ wake wa kitambo, kiasi cha mmoja wa viongozi
wa kundi hilo, Kiboya kupora kipaza sauti na kutamka Baba Sinta
akimtania Nature, jambo ambalo liliwafanya watu washangilie.
Nature
kabla ya kuanza kuimba alimpandisha jukwaani msanii M 2 P aliyezushiwa
kifo wakati akiwa amelazwa Afrika Kusini sambamba na Man Ngwair. MP
alisalimia na kushukuru kwa dua za Watanzania wakati akiwa taabani
wadini, kwani zimemponya na akatumia fursa hiyo kumuombea swahiba wake
Ngwair apumzishwe kwa amani peponi.
Ndipo
Wanaume wakaanza vitu vyao, wakipiga nyimbo za Sonia, Hakuna Kulala,
Mzee wa Busara, Ladhia, Haipotei, Dance With Me na Jimwage.
|
Jaydee na mama yake |
|
Jaydee akikusanya fedha alizotuzwa |
|
Anaziweka kwenye boksi kabla ya kweneda kumpa mama yake. Alyeshika boksi ni King Kiboya |
|
TK wa M Band... |
|
Maeneo kama haya Mh Sugu huwa si mkali...anajua kutabasamu |
|
Rapa kutoka Ukonga |
|
Alikuwepo...Mgaya Kingoba Mhariri wa Michezo gazeti la Habari Leo |
|
Kutoka kulia Baraka Msilwa, Francis Kifukwe na mkewe |
Wanaume
walipoondoka akaibuka msanii mcheza ngoma za asili huku akichezea
nyoka, Mango Star ambaye aliwaacha watu midomo wazi pale alipokuwa
akimnyonya nyoka upande wa kichwani. Akafuatia mkongwe Komando Hamza
Kelele ambaye kwanza alimpandisha mkewe, Stella John Momose Cheyo
jukwaani kumtambulisha, kisha akaimba nyimbo na Tumetulia.
Ikawadia
zamu ya Profesa Jay, ambaye aliimba Joto Hasira pamoja la Lady Jaydee,
baadaye, Teja, Yahya na Joto tena. Jaydee akateremka na kumuacha Jay
amalizie shoo naye akamalizia vizuri kwa nyimbo za Hapo Vipi,
Nikusaidiaje na Kamili Gado.
Watu
kadhaa waliofika Nyumbani Lounge kushuhudia shoo hiyo walilazimia
kugeuka na kuondoka kwa sababu ukumbi ulikuwa ‘umejaa na hakuna pa
kukanyaga’.
Kwa ujumla shoo hiyo ilipendeza, ilikuwa bab kubwa.
Credit to Bin zubery
----
Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.
Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA
Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.
-------------------
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
INTERNSHIP VACANCIES
GOVERNMENT VACANCIES
NGO'S VACANCIES
GOODLUCK
tunakupenda sana jide mungu akupenguvu zidi ya wasiopenda maendeleo yako
ReplyDeleteJide wewe ni mkali tu dada yetu aminia kwenye gemu kitambo na bado upo juu achana na wajinga hao wanaosemasema hawakuwezi ng'oooo
ReplyDelete