PENNY MCHUMBA WA DIAMOND AZIDI KUKONDA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Stori: Imelda Mtema
MTANGAZAJI wa Runinga ya DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’ ameamua kujikondesha mwili ambapo amefanikiwa kupoteze uzito usiopungua kilo  18 mwilini.

Akizungumza na Weekly Star Exclusive, Penny alifunguka kuwa, kutokana na kuona mwili wake unavimbiana, aliamua kufanya mazoezi maalum ya kupunguza mwili sambamba na kufanya ‘dayati’ ambayo imembadilisha muonekano wake (tazama picha ndogo).
“Nimeamua tu kuubadilisha muonekano wangu wa unene kwani nilikuwa ninazidi kuwa bonge, kweli nimefanikiwa maana hata uzito nimepungua kwa sasa.
“Kabla sijaanza kufanya mazoezi nilikuwa na kilo 85 lakini sasa nimepungua hadi kufikia kilo 67, ni mafanikio makubwa ambayo nimeyapata katika zoezi langu la kupunguza uzito,” alisema Penny ambaye ni ‘ubavu’ wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Kuhusu msosi, kwa sasa Penny asubuhi anakula ‘ma-apple’ mawili au kipande cha papai, mchana anakunywa juisi na usiku anamalizia na saladi ya samaki au kuku, analala.
Global Publishers
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

21 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tayari umeukwaa ucjidai kujikondesha.nenda Angaza ujijue afya yako.

    ReplyDelete
    Replies
    1. hahahahahahahaa daaaah!!!

      Delete
    2. Mdauuuuu umeuaaaaa!nimechekaaaaaa,watu wakikonda Kwa stress au mambo mengine wanasingizia diet.

      Delete
  2. chezeyaaa stress za movie ya china....hakuna cha diet..diet yake daimond..aseme kweli alikuwa hali halali kulia tu kisa dai..wema unamkondesha mwenzie..kiukwl ulivyokuwa bonge ulikuwa mzr hapo unaonekana sio diet umepungua kwa mawazo ya mapenzi..pole ila nenepa kdg hapo umezeeka na huo mkorogo mbona umevurungwa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. umeonaaaa eeeeeeeeee angejizoelea tu maana mwenzie anatafuta umaarufu kwa kutembea na mastaa asipofanya hicyo nyota yake itaporomoka sasa yeye peny anajina gani mjini atajutraaaaaaaaaaa

      Delete
  3. Anatia hurumaaa, hakuna diet ya kutoa kilo 18 kwa muda mfupi hivo, huyu lazima ni stress za movie ya Domo na Wema au Ngoma. Aanzie Angaza then mengine baadae.

    ReplyDelete
  4. kupungua kilo 18 ndani ya miezi miwili kwa tizi na diet? acha kutuzingua...basi vimodo wangekua wengi

    ReplyDelete
  5. Aaahhh hizo ni stress na depression za maisha hana lolote......kwanza alivyokuwa bonge ndio alikuwa anapendaza........ama inawezekana ikawa ngoma vile vile.....anamdanganya nani????????.......nyoko zakeeee

    ReplyDelete
  6. amevurugwaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwiiiii kwiiiiii kwiiiiii mnanimaliza huku japan!

      Delete
    2. kasnuriwa kabisaaaaaa hahahaha

      Delete
  7. asugue gaga aende angaza akajue wats up jumlisha bwana alivyo zipu waz na c alisema hatumiagi puto halooooo wakianza dondoka wasanii itakuwa km umepuliza X-PEL ktk kibanda cha muuza utumbo watadondoka km nzi kudadeki

    ReplyDelete
    Replies
    1. Maaaaaaama Mbavu zanguuuuuuuuu

      Delete
  8. Mahaba niue yanakumaliza!pole.

    ReplyDelete
  9. You put your life into risk kisa pesa na majumba,pole mdogo wangu,utakufa utaviacha,presha panda presha shuka mi Ndo maana Wanaume mastaa siwataki ktk maisha yangu,

    ReplyDelete
  10. Wema Ana mimba ya diamond,nasikia nasikia uko china diamond alimvuruga wema akavurugika.

    ReplyDelete
  11. Penny waganga wanakulia hela yako bureeeeee.

    ReplyDelete
  12. Penny pole usiwaze sana, tafuta vyako kwani hapo ni tress za pesa za diamond wala Sio penzi.

    ReplyDelete
  13. chezeya madame wema

    ReplyDelete
  14. Mh jmn dah......

    ReplyDelete
  15. utajijua mwaka huu na bado utakonda sana tu

    ReplyDelete

Top Post Ad