LADIES:TRUE LOVE MEANS GIVE AND TAKE ..TUNAWAPENDA SANA ILA MSITUGEUZE GARI LA MSHAHARA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mimi ni mwanaume wa miaka kadhaa,,Kilichonipelekea kuleta hii mada ni kwamba kila mwanamke ninayeamua kuwa nae,ananipa majukumu mengi,hata kabla sijamtamkia kwamba nimeamua kuwa nitamuoa,sikatai kwamba kumsaidia mpenzi wako ni jukumu ambalo haliepukiki lakini msaada unaotolewa usiwe ndo kigezo cha uwepo wa mapenzi yetu,kwa kipindi kirefu nimevumilia hili toka kwa wanawake kadhaa lakini sasa naona kama naelekea kushindwa,mimi binafsi najihisi kama nina mkosi vile,kwa heshima yako naomba waeleze wasichana/wanawake kwamba wakati mwingine sisi wanaume tunakuwa na nia kabisa ya kuanzisha uhusiano imara wenye uwezo wa kuzaa ndoa,


ila tunakimbizwa na "mizinga" yao ya kila siku.katika mapenzi kuna kusaidiana,ila naona kama wenzetu wanawake wameona msaada pekee wa kupewa ni pesa,au wao pekee ndo wanastahili msaada,Wanawake wengi huwa wanaharibu uhusiano bila kujua,hakuna asiyekubali kwamba kusaidiana katika mahusiano ni jambo jema linalokubalika,lakini sasa visizidi jamani,si kila siku mtu unakuwa na pesa ya kukupa,na pia ikumbukwe kwamba suala la kusaidiana katika mahusiano si la upande mmoja,sote twawajibika kusaidiana,wanawake wengi baada ya kuwa katika mahusiano huamini kupata mtatuzi wa shida zake zote.mwanaume mwenye nia ya kweli na wewe akianza kukuona unaanza kumgeuza kitega uchumi,taratibu huanza kuzua visingizio vya kutoonana na wewe mwishowe anaishia zake.

Kitu kingine ambacho wanawake hawajui,si kila tatizo unampelekea mpenzi wako,mengine peleka kwa ndugu zako,hivi kila siku mnapotuomba pesa mwafikiri twazitoa wapi?sio wote wauza sembe,wanawake wengine wana kipato zaidi ya wanaume lakini bado hata kile kidogo tukipatacho mwataka,jamani na sie wanaume hatupendwi kuumizwa pasipo sababu,wewe kama ni mpenzi wangu najua wajibu wangu kwamba wahitaji hiki na kile ,sie wanaume hatupendwi kuumizwa pasipo sababu,wewe kila kitu pesa,kwani mimi ndo nazitengeneza?hata kama unahisi ninazo nyingi,basi unadhani zote ni kwa ajili yako?hata mimi nina familia ya wazazi,wadogo zangu nk,nahitaji kuwahudumia,Tuhurumiane jamani,True love means give and take,twawapenda sana wake/wapenzi wetu lakini msitugeuze gari la mshahara,najua tabia hii si kwa wanawake wote,lakini asilimia kubwa ndo hao,naomba kupitia blog hii tujaribu kuwekana sawa,kwa wale ambao wana tabia hizi na mnawajua,waelezeni,mnatuumiza, na ndiyo maana hatuishi kusikia vituko vya kina kaka kuwaachia bili wanawake katika sehemu za starehe,kujifanya wanaenda msalani,kumbe anakimbia kukwepa aibu,kwa maana hela ya kulipa hana
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tengeneza MIDONGE YAO uwape hawasikii hao.

    ReplyDelete
  2. mwanamke wa leo hebu jiulize umemsaidia mara ngapi mpenzi wako au wewe ni chuma ulete?

    ReplyDelete
  3. watu tukisema wanawake wa siku hizi ni mashetan wanakuwa wakali wakt ni kweli

    ReplyDelete
  4. sasa utaona comment za makahaba hapa chini

    ReplyDelete
  5. Heheheeeeee@dah bora umetuwakilisha mdau maana sio issue tena ila ni inshu khaaaaa mizinga hatareeeeeeeeee,au utaskia me naipenda kweli hii iphone5 yako jamani dear siez pata ya kwangu@mmmmmmhhhhh!!!!!?????

    ReplyDelete
  6. YAAN SASA HV TU KUNA DEM HUKU MGODN KAKOLA AMEKAA BAA NA MSHKAJ WAKE MARA CM IMEPOTEA NA WALKUWA WAMEKAA WAWL TU MAJANGA HAYA

    ReplyDelete
  7. Acha kucopy kwa sinta blog ww

    ReplyDelete
  8. kwaani kuna ubaya?
    sintah mwenyewe kakopi chimbo!

    ReplyDelete
  9. Mwwenzenu na makario makubwa mpaka kero

    ReplyDelete
  10. ndiyo imekuwa tabia yao hiyo kaka, usipotoa mkwanja wanakuona haufai, tabia chafu sana hiyo, sbb wengi wenye mkwanja wa kutoa ovyo ovyo, ni either mafisadi au wauza sembe, na hao wako kila mahala wikitongoza huyu yule, na gonjwa lipo, wengi wamelisahau hilo.

    ReplyDelete

Top Post Ad