Mchawi Mtanzania Amuibia Mfanyabiashara Mkenya Milioni Tisa, Afungwa jela Miaka 3,kenya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mchawi kutoka Tanzania amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu nchini Kenya kwa kumlaghai mwanamke mfanyabiashara mkenya na kumuibia shilingi milioni tisa.

Mchawi huyo alimhadaa mama huyo kuwa kwa kupitia njia za kichawi angeweza kuzifanya pesa hizo kuwa maradufu yaani milioni 18.

Bwana Amos Chipeta pia ataongezwa kifungo cha miezi tatu kwa kupatikana na vifaa vinavyoumiwa kufanya uchawi kama vile chupa, visu na ngozi ya Paka.

Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Nation, Chipeta alihukumiwa pamoja na mwenzake bwana Peter Christopher aliyepatikana na hirizi zinazotumika kufanyia uchawi.

Bwana Chipeta alimlaghai Bi Catherine Njeri hela zake tarehe tofauti tofauti kati ya mwezi wa Agosti na Decemba 2012 baada ya mwanamke huyo kuwaendea na kumwomba wazifanye pesa hizo ziwe maradufu

Walijitetea kwa kusema kuwa mwanamke huyo aliwaendea ili wampe nguvu za kichawi aweze kuwashinda wapinzani wake wa kisiasa

Maafisa wa polisi walipata hirizi hizo na vifaa walivyotumia kwa uchawi mwezi Februari 1, 2014 katika nyumba ya kukodisha iliyo kando ya barabara ya Juja viungani mwa mji mkuu Nairobi.

Hakimu aliyesikiliza kesi hiyo alisema kuwa wanaume hao waliona mwanamke huyo kuwa mjinga na basi kumnafiki kwa urahisi na kuwa hawana majuto au toba.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hapo minao wote wachawi,nae huyo mwananke alienda kufanyann kama nayeye sio mwanga we pesa kuanzia lini zinakuwa maradufu,hapo wote wafungwe

    ReplyDelete
  2. wakenya acheni ubaguz, ht uyo mama nae mwanga

    ReplyDelete

Top Post Ad