Rose Ndauka na Charlz Baba "BIFU" Zito

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ni dhahiri kuwa sasa , staa wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka na Rais wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘ Chaz Baba ’ wapo kwenye bifu zito. 

Habari kutoka kwa chanzo chetu zinasema kuwa , chanzo cha bifu hilo ni fedha , ambapo Rose alikodisha gari la Chaz Baba kwa ajili ya matumizi yake lakini akalirudisha likiwa limeharibika na kumuomba Chaz alitengeneze kisha angemlipa fedha zake, lakini hakufanya hivyo . 

Staa wa filamu za Kibongo , Rose Ndauka “Alikodi gari kwa Chaz , lakini aliporudisha lilikuwa bovu, akamuomba Chaz alitengeze angemlipa , baada ya hapo akaingia mitini . Chaz alikasirika sana, maana hata Rose alipopigiwa simu alikuwa hapokei .

“Imefikia hatua Chaz ametoa kiapo kibaya , amesema hata akifa, maiti yake isizikwe mpaka Rose alipe fedha zake kwanza , ” kilitiririka chanzo hicho. Akizungumzia ishu hiyo , Chaz alisema , kitu alichokifanya Rose si kizuri na kamwe hawezi kumsamehe mpaka amlipe fedha zake . 

Huyu hapa anafafanua zaidi : “Unajua Rose alikuja kwangu na kukodi gari yangu aina ya Toyota Noah , akarudisha likiwa halitamaniki kabisa , nilipomwuliza akasema walipata ajali , nikamtaka akalitengeneze, akasema hana pesa kwa hiyo nitengeneze atanilipa .

Rais wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘Chaz Baba ’ “Tangu siku hiyo sijaona simu yake wala meseji, hata nikimpigia hapokei . Nimeingia hasara ya kwenda kutengeneza kwa shilingi laki tano, pesa yangu inaniuma , nataka anilipe . 

“Hata kama nikifa leo , maiti yangu isizikwe mpaka Rose alipe haki yangu kwanza . Akitangulia yeye utaratibu utakuwa hivyo sitokubali azikwe hadi ndugu zake wanilipe fedha zangu, ” alisema Chaz Baba .

Baada ya kupata habari hiyo Risasi Jumamosi lilimhoji Rose kulikoni ameshindwa kulipa deni la watu hadi mdai anatoa kiapo kibaya kama kile,akaruka vikali.

“Ni kweli kabisa mimi nilikodi gari ya Chaz nikawa natembelea na ilivyokuja kuharibika nililitengeneza mimi na kwenda kumkabidhi lakini hakuridhika na namna lilivyotengenezwa ndiyo maana anasema ananidai lakini mimi sijui hilo deni , ” alisema Rose .
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwa hiyo nyinyi watu wa bongo movie haya magari mnayotanulia hapa mjini mnakodi,basi hizo filam haziwalipi,mnatoa filamu kila mwezi,inakuwaje mshindwe kununua gari ya million saba,mnavyoishi uko instagram watu wanadhani mna maisha mazurii,kumbe ndio maana hamuishi kupigaana majungu

    ReplyDelete
  2. Mh .... shida tupu

    ReplyDelete
  3. Kaaazi kweli kweli

    ReplyDelete
  4. ustaa kazi kudadeki mtu ka mm unanletea usenge ka huo lazma nkufire tena bila mate

    ReplyDelete
  5. ustaa kazi kudadeki mtu ka mm unanletea usenge ka huo lazma nkufire tena bila mate

    ReplyDelete
  6. Out of topic,Jamani kila afanyalo lulu Elizabeth ,instagram penny ex hawala Wa diamond anaiga?wanashindana AMA ?Huyu kapiga picha shelf la viatu Leo penny nae kapiga picha shelf lake la viatu,mambo Mengi Tu,mi nahisi Ni beef la chini kwa chini maana before hawa wadada walikuwa mashosti,penny,lulu na Yule binti Wa kijaluo Wa meya,sasa mmoja wao akachepuka na bwana Wa mmoja ktk kundi,Huyo kaka Ni muuza sembe anahela ka mchanga,sasa baada ya
    Mwenye bwana kujua anaibiwa akaenda kushitaki.....Hivi urafiki Wa kibongo mpaka mshehe bwana?Ujumbe,ushoga bongo kaziiii

    ReplyDelete
  7. We nae ushamba tu na kuwa na roho ya msamaha kwenye hii dunia tunafanyiwa mengi wewe gari tu kuharibika vipi yule mama kachuma na mumewe mali akafariki ndugu wakamtoa nje na watoto hana pakulala na anasamehe.samehe songa mbele mungu atalubariki zaidi sio viapo hata ukifa bado unakinyongo na Mungu nae akigoma kutusamehe maovu yetu itakuwaje..sijapenda

    ReplyDelete

Top Post Ad