Uongozi YANGA wamchana Ridhiwani KIKWETE…wadai sio Mwanachama wao

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Uongozi wa Yanga umesema Mwenyekiti wa Kamati ya ujezi wa jengo la Mafia, Ridhiwani Kikwete siyo mwanachama wa klabu hiyo kwa kuwa hajalipa ada yake kwa miezi sita mfululizo.

Katika taarifa yake iliyotolewa jana kwa  vyombo vya habari na kusainiwa na Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto ilieleza kitendo cha Ridhiwani kupinga hatua ya Wajumbe wa Bodi ya Udhamini na wanachama wa Yanga kwa pamoja kumuongezea muda wa mwaka mmoja, mwenyekiti wao, Yusuf Manji hayana uzito kwa kuwa siyo mwanachama.

“Ridhwani Kikwete hajalipa ada zake za uanachama kwa miezi zaidi ya 6 mfululizo na kwa mujibu wa Katiba ya Yanga ibara ya 13 kipengele cha pili ambacho kinasema kuwa endapo mwanachama hajalipa ada yake kwa muda wa zaidi ya miezi sita mfululizo atakuwa amekoma kuwa mwanachama wa Yanga.”

“Maoni aliyoyatoa hayana uzito wa mwanachama wa Yanga, labda alikuwa akitimiza haki yake ya kutoa maoni kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunaamini kama angekuwa ni Mwanachama hai wa Yanga angetoa maoni yake kwenye Mkutano wa dharura wa Wanachama  uliofanyika Juni Mosi. Pia angeweza kutoa  kwenye kitabu cha maoni ya kupinga maazimio ya Mkutano huo kilichowekwa hapa klabuni kuanzia Juni 23  hadi  27, hakuna aliyesaini zaidi ya mwenyekiti, Manji.

“Niwakumbushe wanachama wa Yanga sehemu ya kuchangia maoni yao ni kwenye vikao vya Wanachama na siyo kwenye vyombo vya habari,  wasitafute umaarufu kwa njia za kubomoa kuliko kujenga wala wasiwadhalilishe waliojitosa kwa hali na mali kuisaidia Yanga kuwa bora kama Mama Fatma Karume wenye historia ndefu Yanga, tunaona ni sawa na udhalilishaji kwake, kwa kweli inasikitisha sana.

Taarifa hiyo ya Yanga imekuja ikiwa ni siku moja baadaya Ridhiwani kukaririwa na gazeti hili akisema haridhishwi na mambo ya migogoro ya kikatiba yanayoendelea ndani ya Yanga.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu naye Kilaza. Bichwa looote limejaaa maji kisa eti babake ni Rais wa Nchi. Hana lolote kazi kutukana viongozi wenzie.

    ReplyDelete
  2. akili ndogo, kumbe siyo mwanachama, aachane na yanga aende simba msaliti huyu.

    ReplyDelete

Top Post Ad