Kama Mbowe Anataka Watanzania Waandamane Basi Aitangulize Mbele Familia yake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kuna vitu ukisikia vinatamkwa na mtu mwenye mamlaka na anayesimamia sheria inakuongzea hasira. Leo akihojiwa na BBC DCI amesema ikiwa Mbowe anataka watananzania wamuunge mkono kwenye maandamano yake atangulize familia yake vinginevyo watanzania wajue maandamano hayo ni kinyume cha sheria.

Uhitaji mganga wa kienyeji kujua huyu anatumika na Ccm. Maneno hayo yalisemwa na Nape akiwa Pwani, sasa ili kuwafuruhisha mabwana zake anatumia maneno yale yale huku akijua anapaswa kutumia sheria na siyo mipasho. Sasa atueleze ikiwa Mbowe atatanguliza familia yake maandamano ni halali?

Aliwahi kuona Mbowe ametangaza maandamano alafu yeye akabaki nyuma? Kama yeye anaongoza maandamano utasemaje hawezi kutanguliza familia? DCI naye atangulize familia yake CCM au awe anavaa sare za chama hicho ofisini tumjue kabisa!
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ni kweli kabisa, atangulize familia yake. Kule Arusha mwaka jana waliwachochea watu kuandamana halafu wao wakalala mbele na kuwaacha 'wajinga' waandamane, wakapigwa risasi watu watatu wakafariki, wakadanganya watasaidia familia zao, mpaka leo hakuna msaada wowote ule waliotoa zaidi ya blah blah na kutafuta kick tu mjini. Safari hii katu HATUDANGANYIKI!!!!

    ReplyDelete
  2. Hawa chadema wanafufanya sisi wananchi kama mabwege, wanaandaa maandamano halafu wao hawashiriki wanatuacha tupigwe virungu na mabuti ya polisi, safari hii mbele atangulie mbowe na mkewe na watoto, afuate tundu lisu na mkewe na watoto, aje slaa na mchumba'ke na watoto, awepo pia mnyika, kifupi viongozi wooooooote watangulie mbele ndipo na sisi tutawafuata, ili kama ni virungu na mateke tupate wote. Sana sana wao ndio watakao faidika na hayo maandamano, wengine tunafuata mkumbo tu ili kuipitisha siku ipite.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyo Mbowe unaemtaja kwani yupo? Kaenda SAUZI, nyinyi wajinga andamaneni mkione cha moto, akirudi atakuja hospitali kuwapeni pole na kutoa rambi rambi kwa wafiwa ikibidi. Mheshimiwa Pinda alishasema WAPIGENI, TUMECHOKA. Kazi kwenu wenye masikio ya kufa, yasiyosikia dawa.

      Delete
    2. kweli msemao. hawa watu sio, me maandamano ya arusha nilikuwepo niliumia kisigino wkt nakimbia basi hadi leo sipo sawa. hata ela ya hospitali kila nikiwafuata wanipe ela ya dawa wananikwepa. msiwasapoti hawa watu sioooooooooooooo kabisaaaaaaaaaaa. nina ushaid nao na sataki chama chchte nimekoma

      Delete
  3. Mie chadema lakini kwenye maandamano sijii.. Ng'oo

    ReplyDelete
  4. Watu mmeanza kuelewa

    ReplyDelete
  5. Serikali mnakosea sana mnazidi kuupa umaarufu mbowe.

    ReplyDelete
  6. mlichotakiwa mngeamwacha aandamane tu halafu ila mnahakikisha usalama mwisho wa siku wanarudi nyumbani. lakini hivi mnavyozuia ndio mnazidi kumpaishaa!!!

    ReplyDelete
  7. Anonymous 4.18 wewe una akili na unafikiria mbali.ila serikali ya ccm na jeshi la polisi wote kule ndani ni mbumbumbu tu hakuna mwenye akili na yote hii ni matokeo ya kuchukua watu waliofeli shule ndio wanakuwa polisi.wewe unategemea nini hapo wakikutana na watu wenye akili na uwezo wa kufikiri kama viongozi wa chadema?kwani ni mara ngapi polisi walishaingizwa mkenge na chadema na kweli wakaingia?!wote pale hakuna mwenye akili wala hata uelewa wa sheria wanazozisimamia....

    ReplyDelete
  8. Uliyeleta habari hii ni kipofu wa akili,nenda ukamiminwe marangu!

    ReplyDelete

Top Post Ad