Muhongo Aongeza Utata Ufisadi wa Mabilioni ya IPTL

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wakati utata wa kuchotwa kwa fedha katika Akaunti ya Escrow iliyofunguliwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kutokana na mgogoro baina ya IPTL na Tanesco ukiendelea kuzua maswali, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema fedha hizo hazikuwa za Serikali.

“Hizo fedha hazikuwa za Serikali, Tanesco ilitakiwa kulipa Capacity Charge (gharama za uwekezaji) kwa IPTL kama inavyolipa karibu Sh27 bilioni kwa kampuni nyingine zinazozalisha umeme,” alisema Profesa Muhongo.

Itakumbukwa kuwa, kutokana na mgogoro wa IPTL na Tanesco akaunti hiyo ilifunguliwa ili fedha ambazo Tanesco ilipaswa kuilipa IPTL kwa ajili ya Capacity Charge ziwekwe kwenye akaunti hiyo hadi mgogoro huo utakapomalizika.

Kwa kuwa malalamiko yalikuwa kwamba, fedha ambazo Tanesco ilikuwa ikiilipa IPTL zilikuwa nyingi kuliko ilivyostahili, ilitarajiwa kwamba baada ya kesi iliyofunguliwa Marekani kuamuriwa, ingepatikana njia kukokotoa gharama halisi na sehemu ya fedha hizo kurudi Tanesco.

Sehemu ya taarifa kwa umma iliyotolewa na Ofisi ya Uhusiano Tanesco Makao Makuu, Jumanne iliyopita kufafanua taarifa zilizokuwa zimeandikwa juu ya hukumu hiyo inasema: “Mahakama hiyo (ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji) haikutangaza aliyeshinda wala kushindwa.

“Ilichofanya ni kutoa muda wa miezi mitatu kwa pande zote mbili, (Standard Charted Bank Hong Kong (SCB-HK)) na Tanesco kwenda kukubaliana nje ya Mahakama… kwa sasa kuna mazungumzo yanayoendelea kuhusu taratibu za kukokotoa gharama halisi.

“Hivyo basi, kanuni itakayokubaliwa na pande hizo mbili ndiyo itakayosema SCB-HK alipwe kiasi gani ambapo ilitarajiwa angelipwa kupitia fedha zilizokuwa Escrow.”

Profesa Muhongo alipoulizwa iwapo Serikali inaitambua SCB- HK na hukumu iliyotolewa na Mahakama hiyo ya Kimataifa, alisema kwa kifupi: “Kwani sisi tunaendeshwa na sheria za Marekani? Je, hao wabia wengine wanamtambua SCB-HK?”

Pia hakutaka moja kwa moja kukiri kuwa Serikali ndiyo iliyotoa fedha hizo na kuzitoa kwa Pan African Power Solution wala kukanusha taarifa hizo, badala yake alisema swali hilo waulizwe wahusika katika suala hilo.

Chanzo:Mwananchi
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyo ndio mwizi namba moja wa pesa za escrow ndio maana kila siku anajikanyaga na kuibua issue mpya.Muhongo utazitema tu pesa zetu kibaka wewe

    ReplyDelete

Top Post Ad