Albino Wamepigana Ngumi na Mateke Wakigombea Kuingia Kumwona Rais Jakaya Kikwete, Ikulu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino), wamepigana ngumi na mateke wakigombea kuingia kumwona Rais Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam. Tukio hilo la aina yake lilitokea jana majira ya saa nne asubuhi ambapo lilianzia kwenye eneo la mapokezi Ikulu mara baada ya walemavu hao kukaguliwa na kuwekwa kwenye chumba maalumu cha kupumzikia wageni. Baada ya muda, ofisa wa Ikulu alifika kwenye chumba walipokuwa walemavu hao akiwa na karatasi yenye orodha ya watu 15, ambao ndio waliopaswa kumwona Rais. Kila ofisa huyo alipokuwa akisoma jina, mhusika alitoka nje ya chumba hicho tayari kwa kwenda kumwona Rais. Baada ya ofisa huyo kumaliza kusoma majina hayo, alisema: “Hawa ndio wanaokwenda kuwawakilisha kwa sababu hamuwezi kuingia kundi lote hili.”
Wale wengine walioachwa hawakukubaliana na hali hiyo basi vurugu ndio likaanzia hapo!
Nini maoni yako kuhusu hili
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Watu wapo busy kujaribu kuhamasisha kuokoa maisha yao ila wanataka kuuana wenyewe sasa.. dah!

    ReplyDelete
  2. Hii kali ila inaonesha jinsi walemavu hawa walivyo na machungu kiasi kwamba kila moja anatamani aeleze shida ya albino yeye mwenyewe. Poleni sana Albino Tupo pamoja kuwatetea mpaka mwisho

    ReplyDelete
  3. Wangeachwa wakamuone kwani ni wengi kiasi gani hao, mbon aulaya anakuatana na wanatanzanai wengi tu kwa maramoja, na nimara nagpi mheshimiwa ameonana nao kiasi cha kuamua kuwazuia.

    ReplyDelete

Top Post Ad