Leo ni Zamu ya Kuwajua Mastaa wa Bongo Wanaoongoza Kutukanwa Mtandaoni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kwa upande wa wale ambao wanashika nafasi za juu kwa kutukanwa, wapo wengi lakini leo tutawazungumzia wahanga watatu.

Kajala Masanja:

Tangu aingie kwenye bifu na Wema Sepetu, kuna kundi ambalo linajiita Team Wema limekuwa likimshambulia kwa kumtukana na kumshutumu kwa mambo ambayo mengine hayana ukweli.

Hata hivyo, Kajala anaonekana kuwa mstaarabu kidogo kwani licha ya kutukanwa mtandaoni, yeye amekuwa mkimya akijua kujibizana na watu hao ambao wala hawana majina ni sawa na kuzidi kujichafulia.

Elizabeth Michael ‘Lulu’:
Huyu naye ni mhanga wa matusi mtandaoni. Kuna kundi la watu ambao linaonekana kuwa na chuki dhidi yake, huenda kutokana na mafanikio aliyonayo akiwa kwenye umri mdogo.

Lakini sasa, licha ya matusi anayoyaoga mtandaoni, amekuwa mvumilivu wa kuyaacha yapite. Watu wake wa karibu wanaeleza kuwa, licha ya kutukana sana mwenyewe wala hajui kwamba anatukanwa kwani si mtu wa kufuatilia nani kasema nini kibaya juu yake

Wema Sepetu:

Kama ilivyo kwa Kajala, huyu naye anashambuliwa sana na Team Kajala. Hawa ni watu ambao wamejitenga kuhakikisha wanamkosesha amani staa huyu.

Amekuwa akitukanwa kwa mengi lakini kwa kuwa anajua ustaa ni kama jalala, huwa hajali na anachukulia poa.

 Ni mara chache sana amekuwa akinyanyua mdomo wake kuwajibu wale ambao wamekuwa wakimsema vibaya sambamba na kumtukana.

Kwa uchache hao ndiyo mastaa ambao hivi karibuni wametia fora kwa

 kutukana na kutukanwa mtandaoni.

Tahadhari

Mastaa ambao ni wepesi kutukana mtandaoni  wajue kwamba endapo Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete atasaini ile sheria ya makosa ya mtandaoni ya mwaka 2015, watajikuta wanaenda jela hivi hivi.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad