ZITTO KABWE na Prof MARK MWANDOSYA Wapeana za Uso laivu Bila Chenga...Zitto Aanza na Mwondosya Akajibu..Soma Hapa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Majibu ya Prof. Mwandosya kwa Mhe. Zitto Kabwe kwenye post yake Instagram

ZITTOKABWE: Prof. Mark Mwandosya aliwahi kuwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wakati wa uongozi wa Rais Benjamin Mkapa. Mashirika yote ya Umma , takribani, katika Wizara hii yaliyobinafsishwa zoezi la ubinafsishaji liligubikwa na tuhuma za ufisadi na hata kuchukuliwa upya na Serikali. Shirika la Ndege la Taifa lilibinafsishwa chini ya Mwandosya na likafa. Kitengo cha makontena katika Bandari ya Dar Es Salaam kilibinafsishwa kipindi hiki na kuleta maneno mengi sana. Mchakato wa kubinafsisha Shirika la Reli pia ulianza kipindi hiki. Ubinafsishaji ulioleta maneno mengi zaidi ulikuwa ni wa Kampuni ya simu (TTCL) kwa MSI detecon na Celtel International. Prof. Mwandosya binafsi alipata tuhuma na mtoto wake kusomeshwa na watu waliouziwa kampuni hii kwa bei ya chee. Masuala haya yaliandikwa na vyombo vya habari miaka ya kati ya 2001 na 2005. Prof. Hana budi kufafanua haya mbele ya umma ili kujiridhisha na uwezo wake wa kupambana na rushwa na ufisadi.

MARKMWANDOSYA: Zitto, salaam. Hongera pia kwa kuwa kiongozi wa ACT na hongera kwa kazi kubwa unayoifanya kueneza itikadi ya chama chako. Ni jambo zuri katika kukuza demokrasia ya nchi yetu na hasa kukuza uzalendo. Siku zote nimekuelezea kama kijana ambaye hakika utakuwa tegemeo la Taifa letu, na hili nimekuambia mara nyingi. Nimeona vema nifafanue yale ambayo umeyataja katika post yako. Niliyatolea maelezo ya kina miaka mingi iliyopita lakini nadhani utafiti sio moja ya maeneo tuliyo na nguvu nayo kwa hiyo umeyafufua bila kuyafanyia utafiti au kutaka upate ufafanuzi kutoka kwa mhusika. Nianze na hili suala la ubinafsishaji kwa ujumla wake. Inawezekana wakati huo ulikuwa bado shule ukiwa mwanafunzi. Pamoja na nia njema ya kuanzisha mashirika ya umma, hatimaye yalikuja kuwa mzigo mkubwa kwa hazina yetu, maana yake kwa wananchi.

Asilimia kubwa yalitegemea ruzuku ya serikali na baadhi yalikuwa mufilisi. Teknolojia ilikuwa imebadilika sana na ili kuyafufua ingeigharimu serikali na umma wa Tanzania kiasi kikubwa sana. Uchumi wa nchi wakati ule usingeweza kubeba mzigo huo. Ndipo Chama, wakati ule kiliporidhia serikali ibakie na shughuli zake za msingi za Utawala, Ulinzi na Usalama, na Usimamizi wa ujumla wa uchumi. Maamuzi yafuatayo yakachukuliwa: Kwa upande wa shughuli za serikali zenye sura ya kibiashara, idara husika zikageuzwa kuwa wakala wa serikali, zikifanya kazi kwa uhuru zaidi chini ya Bodi zao. Kuhusu mashirika na kampuni za umma zenye mwelekeo wa kiniashara, ilikubalika zirekebishwe na hatimaye zibinafsishwe. Ndipo kilipoundwa chombo maalum kisheria kilichokuwa na mamlaka kamili ya kubinafsisha mashirika ya umma. Chombo hiki, Tume ya Kurekebisha Mashirika ya Umma(Parastatal Sector Reform Commission, PSRC), kilikuwa chombo huru kikiwa chini ya Ofisi ya Rais, Mipango. Kiliwekwa hapo kwa sababu mamlaka yake yalikuwa Mtambuka, na vyombo husika vilikuwa kwenye sekta mbalimbali. Kwa hiyo sekta husika na Wizara husika, pamoja na kuitwa PSRC wakatii wa majadiliano yaliyohusu mashirika yake, hazikuwa na mamlaka ya kisheria kuhusu ubinafsishaji. Kwa mujibu wa Sheria ya Kurekebishaashirika ya Umma,mara shiriks lilipoorodheshwa na PSRC, liliwekwa chini ya PSRC ili kurekebishwa na hatimaye kubinafsishwa. Ni vema suala uuuhili likaeleweka.

Pamoja na hayo, nirudie ufafanuzi kuhusu ubinafsishaji wa TTCL, nafanya hivyo kutokana na dhana ya uwajibikaji wa pamoja, ikumbukwe kwamba maamuzi ya ubinafsishaji wa TTCL yalifikiwa na PSRC mwaka mmoja kabla Waziri Mwandosya hajaingia siasa! Hata hivyo suala kubwa ni mabadiliko ya teknolojia tu. TTCL ilikuwa imejikita zaidi kimfumo na kiteknolojia katika teknolojia ya analogue na land lines na simu za mezani ambazo zilikuwa na hata sasa zimepitwa na wakati. Mfumo wake, kiutawala na kiteknolojia ulikuwa katika msingi huo. Teknolojia ya simu za mkononi, na ushindani uliojitokeza ndio hasa umekuwa changamoto kubwa ya TTCL. Hata hivyo mabadiliko makubwa na maendeleo makubwa katika TEHAMA na mfumo mpya wa utoaji leseni katika huduma za mawasiliano umepelekea Tanzania kuwa mbali na kuwa mfano wa kuigwa na nchi nyingi za Afrika.

Katika mawasiliano, Tanzania imekuwa 'Mecca' na wengi wamekuja kujifunza tumewezaje kufanikiwa. Namshukuru Rabuka kwa kuniwezesha kutoa mchango wangu katika maendeleo ya sekta hii. Na ili kuhakikisha kwamba mlaji au mtumiaji wa huduma za kiuchumi hahujumiwi na wakati huo huo mtoa huduma au mwekezaji ana uhakika wa kufaidika na kuweza kutoa huduma endelevu, ndipo vilipoanzishwa vyombo vya udhibiti wa huduma za kiuchumi, (Regulatory Bodies). Nimebahatika kuwa Waziri pekee mwanzilishi na msimamizi wa TCRA, SUMATRA, TCAA, na EWURA. Nimeelezea kuhusu mfumo wa ubinafsishaji hivyo basi ninachoweza kufafanua ni kwamba nilipomaliza muda wangu kama Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, niliacha Shirika la Reli likisafirisha tani laki tisa za shehena kwa mwaka, safari za abiria kwenda Tabora kutoka Dar zilikuwa kila siku, na ATC ilikuwa na ndege mbili aina ya Boeing 737 na mbili aina ya Fokker Friendship.

Tuhuma za mtoto wa Profesa kulipiwa na kampuni moja ya simu hazina chembe yoyote ya ukweli Bwana Zitto. Mtoto ambaye alifuzu uhandisi wa mawasiliano ya simu aliomba kazi ya muda na akapewa.

MARKMWANDOSYA: Kampuni husika ilikanusha tuhuma hizo ambazo zilitolewa wakati wa mchakato wa kugombea uteuzi katika CCM kwa nafasi ya kuwa mgombea wa Urais mwaka 2005. Sasa zinafufuliwa tena na Bwana Zitto wakati wa mchakato huo huo mwaka 2015! Inaeleweka.

MARKMWANDOSYA: Na kwa taarifa kwako Bwana Zitto, kwa kuwa bandari ni kitovu cha mapato ya serikali, ubinafsishaji wa Container Terminal ya Bandari ya Dar es Salaam ulifanywa na PSRC kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha, na siyo Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi.

Namalizia kama nilivyoanza, Zitto ni mwanasiasa ninayemheshimu sana. Mara nyingi naye amenitambua na kunielezea mimi kama mwanasiasa wa kuigwa (role model). Lakini katika siasa tunasema saa 24 ni kipindi kirefu sana, na huwa tunabadilika! Ushauri wangu kwake ni kwamba siku zote kabla hujahukumu sikiliza upande wa pili, kwa kilatini hii ni dhana muhimu inayojulikana kama AUDI ALTERAM PARTEM. Pili ni vema ukazingatia zaidi mambo chanya ya mipango, mkakati, msimamo na itikadi ya ACT. Siasa za majitaka hazimuachi mtu bila doa! Lakini katika kushauri hivyo natambua kwamba "akili ni nywele, kila mtu ana zake" Ramadhan Kareem. Wakatabahu, Mwandosya.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. profesa mchane huyo msaliti, ametumwa huyo!!

    ReplyDelete

Top Post Ad