Ticker

6/recent/ticker-posts

Nampa Kila Anachostahili Mke Wangu Lakini Sina Amani na Ndoa yangu....

Mke wangu nampenda sana kila anachotaka nampa. Yeye ni mwalimu wa msingi. Uwezo wangu wa kifedha si mkubwa lakini nimejitahidi hadi nimemnunulia walau kigari cha kuendea kazini katika jitihada za kumfanya nae ajisikie vizuri mbele za watu.

Mshahara wake ni chini ya laki 5 lakini huwa namwekea mafuta ya shilingi laki 3 kwa mwezi ili aende kazini. Nampa matunzo yote anayotaka kama mke wa ndoa anavyostahili.

Kinachonisikitisha ni dharau anazonionyesha ndani ya nyumba. Akiamua kunitukana inachukua siku tatu kumaliza matusi. Nyumba haina amani naishi kama mhamiaji haramu. Kuna wakati ananiangalia tu na kunisonya bila kumkosea chochote.

Anadai nikisafiri anaishi kwa amani nikirudi anakereka. Kwa kifupi mimi huwa ni mara chache huwa najibizana nae ninapozidiwa na hasira lakini mara nyingi hukaa kimya.

Nimejaribu kujiuliza ni wapi nakosea sipati jibu. Natunza familia vizuri, unyumba nampa, sina vimada na wala hajawahi kunihisi.

Tatizo ni nini? Nisaidieni wadau niishije na huyu mke? Akiugua anajitahidi kuonyesha jamii kuwa simjali anaamka mapemaa anawahi hospitali ili nionekane simjali.

 DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Akiamua kunitukana anatumia matusi na kashfa nzito dhidi yangu. Bado sijamsimulia mtu yeyote kwa ajili ya kulinda heshima ya familia lakini naona kama nazidiwa.

Naombeni ushauri wenu.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

7 Comments

 1. achana nae utafute mwingine wapo wengi wanaitaji mume kama wewe😉

  ReplyDelete
 2. Inawezekana uliforce kuwa nae labda alikua anamtu anampenda kabla yako tafuta mapenzi ya kweli sio pesa

  ReplyDelete
 3. mpeleke kwenye maombi jini mahaba hilo.

  ReplyDelete
 4. Kaka timua huyo c demu kapata kwingine kwa hyo wewe uctegemee kupta heshima kama mume, hata kama humu fikishi kileleni ana pasws kuwa waz ili nawe
  ujue kumbe mke wangu namnyima haki yke,

  ReplyDelete
 5. kama una hasira mchape makofi na mpe likizo aende kwao kwanza hana shukrani sema usipende sana kuwa na kiasi kaka wanawake wengi ukimpa kila kitu upendo anahamishia kwenye pesa na pendo la jweli anahamishia kwingine jitahidi naye umpe chance nayeye yakukujali we mwambie huna pesa ili aifikirie familia nayeye ndo utagundua kuwa kuwa hiyo heshima yakuitwa mke anaistahili au la!

  ReplyDelete
 6. mitihani hiyo kama umezaa nae punguza mapenzi kwake zidisha kwa watoto.

  na kama muislamu ongeza mke wa pili ,sema huyu uwe makini nae asije akakuletea gonjwa ni.
  anaonekana hajatulia

  ReplyDelete
 7. Kimsingi uwe ujeuri kidogo ndugu yangu wanawake hawatabiriki, unaweza kudhani kwa kumnunulia gari atatulia lakini mwenzio hana muda naye
  Kaa naye chini mueleze usivyofurahia maisha yenu kwa sasa tofauti na mipango yenu kabla hamjaoana
  Kama kuna tatizo atakueleza lakini tofauti na hapo piga kuna hakiko sawa, fanya uchunguzi ukiwa tayari kufanya maamuzi magumu

  ReplyDelete
Emoji
(y)
:)
:(
hihi
:-)
:D
=D
:-d
;(
;-(
@-)
:P
:o
:>)
(o)
:p
(p)
:-s
(m)
8-)
:-t
:-b
b-(
:-#
=p~
x-)
(k)