Kosa lililowasimamisha Wabunge Saba wa Upinzani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Bunge jana limeazimia kuwasimamisha vikao wabunge 7 wa kambi ya upinzani kwa kosa la kukiuka sheria na kanuni za bunge na kushinikiza kujadiliwa kwa hoja ambayo imekwisha tolewa maamuzi kinyume na utaratibu wa kanuni za Bunge.

Akisoma maamuzi hayo ya Bunge Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge, George Mkuchika amesema Januari 27.01.2016 wabunge hao walikiuka sheria na taratibu za kuongoza bunge kwa walishinikiza kiti cha spika kijadili hoja ambayo ilikwisha tolewa uamuzi na kiti hicho.

Wabunge waliosimamishwa kuhudhuria vikao hivyo ni Zitto Kabwe, John Heche, Halima Mdee, Tundu Lissu, Godbless Lema, Pauline Gekul na Esther Bulaya.

Azimio la adhabu kwa wabunge hao limetolewa na Bunge chini ya Kifungu cha 30A (1) cha sheria ya Haki Kinga na Madaraka ya Bunge Sura ya 296 na kanuni ya 74 (4) na (6).

Kufuatia uchunguzi huo Bunge kupitia kamati hiyo limeazimia kuwa Ester Bulaya naTundu Lisu wasihudhurie vikao vyote vya mkutano wa tatu wa Bunge la Kumi na Moja vilivyobaki kuanzia tarehe 30 Mei , 2016 pamoja na vikao vyote vya Mkutano wa Nne Spika wa Bunge la Kumi na Moja kwa kuwa walipatikana na makosa ya ukiukwaji wa Kanuni na kuonyesha dharau kubwa kwa mamlaka ya Bunge.

Aidha, Bunge limeazimia kuwa Mhe. Pauline Gekul, Mhe.Godbless Lema, Mhe.Zitto Kabwe na Mhe Halima Mdee wasihudhurie vikao vyote vya mkutano wa tatu wa Bunge kuanzia tarehe 30 Mei 2016.
Adhabu hizo Bunge limeazimia Mhe.John Heche asihudhurie vikao kumi mfululizo vya Mkutano wa Tatu wa Bunge hilo kuanzia Mei, 30, 2016 kwa kuwa alipatikana na kosa moja
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ukiitwa Member of Parliament (MP).. Ni kwamba umepewa Dhamana na Cheo katika Nchi teule. Heshima yako , mazungumzo yako, Daraja yako katika Jamii inakuwa ni teule kivyake. Kwa hiyo uwajibikaji wako na ufanisi wa kazi yako pia unakuwa au unahitajika uwe ni wa hali ya JUU..Kisomo na Busara huwa pia kinachangia kwa kiasi kikubwa kukusaidia lengo hili.. Barazanin na Vijiweni kama utapita inakuwa ni kwa nadra kama siyo kukosekana..Hawa Waheshimiwa husika ni idadi ndogo ya wenye mfano kama wao.. Lakini hatu hii ni mojawapo stahiki iliyo chukuliwa ambayo itakuwa mfano kwa waliobaki na hao wenyewe wapate mwamko kwamba Bunge LINA kANUNI NA uwezo WA KUCHUKUA HATUA INAPO BIDI NA hIVI tUMECHUKUA hATUA ILI IWE ONYO. KWA LENGO LA KUMWAMSHA KIMAWAZO ALIYEJISAHAU... nAPONGEZA KAMATI HUSIKA KWA HATUA HII.. NAPONGEZA WABUNGE KWA KULIUNGA MKONO SUALA ZIMA LA HATUA TEKELEZI INAYODHIHIRISHA NIA NJEMA YA KUTOTAKA KUPOTEZA WAKATI WA CHOCHOTE BAADA YA UAMUZI AU MWONGOZO KUTOLEWA..HII ndiyo njia sahihi ambayo tunaweza kumsaidia JPJM kuendelea kututumikia kwa kasi nzuri zaidi bila kumchosha na hawa watu wenye ni na lengo la kuleta Uvivu na Sabotage ya Gurudumu la maendeleo na kuifanya safari iwe ndefu zaidi....JPJM pamoja sana na Mh. K Majaliwa

    ReplyDelete
  2. Ukiitwa Member of Parliament (MP).. Ni kwamba umepewa Dhamana na Cheo katika Nchi teule. Heshima yako , mazungumzo yako, Daraja yako katika Jamii inakuwa ni teule kivyake. Kwa hiyo uwajibikaji wako na ufanisi wa kazi yako pia unakuwa au unahitajika uwe ni wa hali ya JUU..Kisomo na Busara huwa pia kinachangia kwa kiasi kikubwa kukusaidia lengo hili.. Barazanin na Vijiweni kama utapita inakuwa ni kwa nadra kama siyo kukosekana..Hawa Waheshimiwa husika ni idadi ndogo ya wenye mfano kama wao.. Lakini hatu hii ni mojawapo stahiki iliyo chukuliwa ambayo itakuwa mfano kwa waliobaki na hao wenyewe wapate mwamko kwamba Bunge LINA kANUNI NA uwezo WA KUCHUKUA HATUA INAPO BIDI NA hIVI tUMECHUKUA hATUA ILI IWE ONYO. KWA LENGO LA KUMWAMSHA KIMAWAZO ALIYEJISAHAU... nAPONGEZA KAMATI HUSIKA KWA HATUA HII.. NAPONGEZA WABUNGE KWA KULIUNGA MKONO SUALA ZIMA LA HATUA TEKELEZI INAYODHIHIRISHA NIA NJEMA YA KUTOTAKA KUPOTEZA WAKATI WA CHOCHOTE BAADA YA UAMUZI AU MWONGOZO KUTOLEWA..HII ndiyo njia sahihi ambayo tunaweza kumsaidia JPJM kuendelea kututumikia kwa kasi nzuri zaidi bila kumchosha na hawa watu wenye ni na lengo la kuleta Uvivu na Sabotage ya Gurudumu la maendeleo na kuifanya safari iwe ndefu zaidi....JPJM pamoja sana na Mh. K Majaliwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hiviii, hawa jamaa walitakiwa wawe mabubu au wawe wana cheka cheka wakati wa kuchangia ndio wangeeleweka au!!? maana namkumbuka jamaa mmoja kwenye mada ya escrow yeye akawaambia wenzie wana ashiki majununi!! na baadhi yao wakacheeeka!!
      haya tunasubiri tuone mwisho wa haya yote...

      Delete
    2. sIO MABU BU.. HAWA NAONA WAMESHADATA AU WANAPIGA VITU KABLA YA KUINGIA KUCH NEHI KUCH NEHI WANALETA DRAMA... SI ACT TU

      Delete
  3. lazima wawatoe hao ndio majembe yetu, yanayo watoa jasho bungeni, wamezidiwa mbali wa ccm ndio maana wanatumia nguvu huyo naibu spika ni mwana ccm vp awe upande wa upinzani bora wa mtoe anaonesha ubaguzi wazi wazi, kwa hiyo wabunge wa upinzani hawana haki ya kuongea?

    ReplyDelete

Top Post Ad