Tamko la ACT Wazalendo Baada ya Wabunge wa Upinzani Kufungiwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Baada ya Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge kuwatia hatiani wabunge saba kwa makosa mbalimbali ikiwemo kudharau madaraka ya bunge ambapo wabunge Easther Bulaya na Tundu Lissu wameadhibiwa kutokuhudhuria vikao vilivyobaki vya mkutano wa tatu na vikao vyote vya mkutano  wa nne.

Wabunge Pauline Geku, Halima Mdee, Zitto Kabwe, Godbless Lema wamepewa adhabu ya kutokuhudhuria vikao vyote vilivyobaki vya mkutano wa tatu na Mbunge John Heche hatohudhuria vikao kumi vya mkutano wa tatu. Makosa hayo waliyafanya mkutano wa pili mwezi January.

Baada ya adhabu hiyo kwa wabunge, ACT Wazalendo wametoa tamko lao ambapo wameyazungumza haya……

’Chama cha  ACT Wazalendo kimesikitishwa na kitendo cha ugandamizaji wa demokrasia kilichofanywa na wabunge wa CCM kwa kuwasimamisha ubunge wabunge wa upinzani akiwemo kiongozi wa chama chetu  Zitto Kabwe’

’Katikati ya masikitiko hayo tunafarijika kuona wabunge hao wameondolewa kwa sababu ya misimamo yao ya kutetea maslahi ya wananchi’

’Tungesikitishwa zaidi kama mashujaa wetu hawa wangeondolewa bungeni kwa sababu ya ulevi au wawe sehemu ya wagonga mihuri ya masuala ya hovyo hovyo yanayosimamiwa na serikali ya chama cha Mapinduzi (CCM)’

’Kwa sababu hiyo ya kusimamia maslahi ya wananchi sisi kwetu ni mashujaa na kwa maana hiyo Chama chetu kinaandaa maandamano makubwa jijini Dar Es Salaam kuwapokea mashujaa wa wananchi’
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Act hivi hii ndiyo Tamko au Hotuba yenu..Ni nani huyu aliyeandika hii.. Na kama sikose ukisema "tunafarijika wameondelewa kwa misimamo yao kuwatetea maslahi ya wananchi" mimi mbona sielewi mna maanisha nini... yaani zito anakweja DA GOMA AU MANAAKE PIA SIELEWI... HEBU ZUNGUMZENI KUNYOOSHA MANANE NANI KAADINNKA HII ...KWA PESELI YA UZITO.. HIVYO HIZI KULA ZENU..ACT AKILUDI HAMNA DLAMA YA KISAANI TENA AJILI ACTOR KUCH NEHI..

    ReplyDelete
  2. aCT- Actor kuch nehi... KUCH NEHI... HAKUNA DLAMA TENA... INABIDI UANGALIE USTALABU MWINGINE..BARIDA MWANANGU

    ReplyDelete
  3. aCT- Actor kuch nehi... KUCH NEHI... HAKUNA DLAMA TENA... INABIDI UANGALIE USTALABU MWINGINE..BARIDA MWANANGU

    ReplyDelete
  4. hamna akili ACT hata mkiandaa hayo maandamano eti mkidai mashujaa mashujaa walishatangulia mbele za haki acheni upumbavu msitafute kiki kama walizkuwa wakizitafuta wao na ndio maana wamesimamishwa tena wengine hapo wa akina halima wana mambo ya ajabu haijawai tokea halafu wanajiita wabunge tumieni akili na utashi sio kukurupuka tu nfyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  5. masilahi gani ya kusimamiwa na Halima mdee, masilahi gani ya kusimamiwa na Esta bulaya bado tunahitaji sana elimu ya kutosha kiukweli wanapiga blaa tu hao

    ReplyDelete

Top Post Ad