Imefichuka..Wabunge wa CCM Wapangwa Kumtetea Makonda Bungeni..Mchezo Mzima Utakuwa Hivi..!!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Baada ya taarifa ya Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge chini ya mtani na kaka yangu Kepteni Mstaafu George Huruma Mkuchika kukabidhiwa kwa Spika, Spika ataiweka taarifa hiyo katika ratiba za shughuli za Bunge ili iwasilishwe na kujadiliwa. Tayari Mkuchika na Kamati yake wameshakamilisha taarifa yao tayari kuikabidhi kwa Spika, Ndugu Job Justino Ndugai.

Taarifa hiyo inatarajiwa kuwasilishwa na kujadiliwa kati ya leo au kesho. Taarifa ya Kamati ya Mkuchika itabeba kilichopatika katika mahojiano na Makonda; maoni na mapendekezo ya Kamati. Makonda (Daudi Albert Bashite) aliitwa kuhojiwa na Bunge kupitia Kamati hiyo kwa kulidharau Bunge kupitia kauli zake za kejeli na kiburi alizozitoa juu ya Bunge na Wabunge.

Katika hali ya 'kudhibiti' kauli na mwenendo wa Wabunge wa CCM kuhusu taarifa hiyo, viongozi wa Wabunge wa CCM wameanza kuwapanga Wabunge wa CCM. Kuwapanga huko kunaratibiwa na Katibu wa Wabunge wa CCM, Ndugu Jason Rweikiza. Rweikiza, kwa mujibu wa taarifa toka Dodoma, anawataka Wabunge kupongeza hatua ya Makonda ya kuomba msamaha kwa barua.

Imeelekezwa kuwa kama Rweikiza na timu yake watakwama kuwapanga Wabunge wa CCM kuhusu taarifa hiyo, basi kutalazimu kuwepo kwa Kikao cha Wabunge wote wa CCM almaarufu kama Party Caucus ili Wabunge waandaliwe na utaratibu wa kuwamulika mjadala utakapoanza uwekwe. Maandalizi ya haraka ya Caucus yatafanyika.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mwacheni achape KAZI.
    Katupunguzia mateja bhana!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Jitambue jithamini jiongeze

      Delete
  2. Ukweli unauma-jamani, hebu wajiulize wao wenyewe kwanza, hivi sio kweli kwamba huwa wanalala bungeni?? Nakumbuka spika mmoja aliwahi kusema kusinzia unaruhusiwa, ilimradi usikorome tehetehe

    ReplyDelete
  3. Makonda anamakosa mengi. Kufiji vyeti.
    Kulidharalisha bunge
    Kuvamia kituo cha habari
    Halafu anajadiliwa
    Hivi ccm mna nia ya kufusta sheria za nchi au bao la mkono bado mnalitembeza usiku kweupe bila haya.
    Kunawatu Raisi hakuwapa hata muda akawafyeka hadharani kweupe
    Mtoto Makonda Msukuma anajadiliwa baada ya haya yote sababu ni msukuma?
    Mkasi kwa mgogo, msukuma dahabu?
    Hii nchi yetu vipi.uoga sababu rsisi hatski kusmriwa, kila kiongozi anaufyata. Ni viongozi gani? Kama sheria ni moja, gugumizi la viongozi wote linakuwaje? Haki itendeke kwa kila Mtanzania bila kujali ukabila na ukaribu wa Raisi.Raisi ni binadamu kama binadamu mwingine yeyote na alijue hili. Si Mungu. Wote tunakwenda kanisani kuomba upeo ili tufanye kazi bila upendeleo wowote. JeRaisi wetu analijua hili. Usawa, haki, vitumike. Busara, hekima kwa viongozi lazima vitawsle kazini. Kama umetangaza kufyeka fyeka basi.

    ReplyDelete

Top Post Ad