TTB Yaitangaza Tanzania Eneo Bora la Utalii Duniani..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Bodi ya Utalii Tanzania(TTB) imejipanga kuitangaza Tanzania kama eneo bora la utalii katika maonyesho ya Kimataifa ya Utalii yajulikanayo kama Internationalle Tourismus Borse (ITB) yaliyoanza rasmi jijini Berlin Ujerumani katika eneo la Messe Berlin na kuhudhuriwa na jumla ya nchi 187 kutoka kote duniani.

Mratibu wa ushiriki wa Tanzania katika maonyesho hayo ambaye pia ni Meneja Masoko wa Bodi ya TTB, Geofrey Meena amesema TTB imejipanga vilivyo kuitangaza Tanzania kama eneo bora la utalii duniani ambapo pamoja na kuendelea kuvitangaza vivutio v kama vile mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro, Hifadhi  za Taifa, fukwe na maeneo mbalimbali ya kihistoria.

Pia mwaka huu mkazo umewekwa katika kutangaza ushahidi wa nyayo za binadamu wa kale (Zamadamu) uliovumbuliwa miaka milioni nne iliyopita katika eneo la Laetoli lililoko takribani kilometa 45 kusini mwa Olduvai Gorge.

“Pamoja na kuvumbuliwa kwa fuvu la anayesadikiwa kuwa ni binadamu wa kwanza kabisa duniani huko Olduvai Gorge Ngorongoro, lakini katika kuendelea kudhihirisha kuwa Binadamu wa kwanza aliishi Tanzania tumeamua katika maonesho ya mwaka huu kuja na ushahidi unaoelezea ukweli huo kwamba Binadamu asili yake ni Tanzania,” amesema Meena.


----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad