Kikwete ni Rais Bora au Watu Wanamkomoa Rais JPM?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kikwete amekuwa kipenzi cha watu ghafla, kila anapoonekana hushangiliwa na kusifiwa, ilianza pale Msigwa alipotamka bungeni kuwa wamemmiss, ikaja alipoingia bungeni kumsindikiza mkewe, lakini pia hata juzi alipokuwa akiingia uwanjani katika sherehe za Muungano.

Marais wastaafu hatukuwahi kuona wakishangiliwa, si MKAPA, wala MWINYI hata Baba wa taifa sikumbuki kuona akiingia sehemu baada ya kustaafu na watu wakaanza tu kumshangilia bila sababu. Mara nyingi mzee Nyerere alishangiliwa hasa wakati wa speech zake tamu na zenye kugusa.

Swali linaloumiza kichwa, Je huyu Kikwete aliyelaumiwa kila kona wakati wa miaka yake ya URAIS ni kweli kwamba hatukutambua ubora wake wakati huo, au tunamshangilia ili tu kumuudhi na kumkomoa JPM ambaye amejipambanua kuhakikisha anarekebisha yale yaliyofanywa na kikwete?

Nimeshindwa kung'amua kimsingi hasa shangwe za wananchi kwa Kikwete, au wanamuinjoy tu, kama wasemavyo waswahili??
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ni unafiki tu. Kwangu mimi hakuna Rais alie bora na kutuletea heshima Tanzania kwa muda mfupi tu aliokaa madarakani kama Magufuli. Mnalalamika sasa lakini mipango ya Magufuli yakikamilika ndio mtakapojua. Magufuli oyeeeee daima. Hapa kazi tu

    ReplyDelete
  2. unafiki unakuponza wewe na si wantanzania wote!!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad