DONALD Trump si Mtu wa Mchezo Mchezo...Aaanza Kuwashughulikia Waislam

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais wa Marekani, Donald Trump ameweka masharti mapya ya maombi ya hati za kusafiria kwa mataifa sita ya Kiislamu na wakimbizi duniani.

Moja ya masharti hayo ni kuwa anayeomba visa lazima awe na uhusiano na mtu mwenye ushirikiano wa kibiashara na Marekani.

Nchi zinazoguswa na masharti hayo ni pamoja na Iran, Libya, Somalia, Sudan Syria na Yemen.

Ujumbe kuhusu masharti hayo umetumwa katika balozi zote za nchi hizo.

Masharti hayo mapya yameanza kutekelezwa jana na yanagusa pia mahusiano ya kifamilia kama mzazi, mkeo ama mumeo, mtoto wa kiume ama wa kike aliye Marekani.

Masharti hayo yanatolewa baada ya Mahakama Kuu nchini Marekani kusitisha  kwa muda agizo la Rais Trump  la kuzuia nchi za Kiislamu kuingia Marekani, zuio ambalo lilikosolewa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. atawashughulikia waislam wakati juzi tu alikua arabuni anaomba pesa kwa waislam. labda atashughulikiwa yeye

    ReplyDelete

Top Post Ad