MBOWE Afunguka Mazito........Aitaka Serikali Iweke Hadharani Ripoti zote Mbili za Madini ili Kila Mtu Azisome

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Serikali imetakiwa kuweka hadharani ripoti zote mbili za madini zilizoandaliwa na kamati zilizoundwa na Rais John Magufuli kuchunguza uendeshaji wa sekta ya madini nchini.

Hayo yamesemwa jijini dar es Salaam leo na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, katika mkutano na vyombo vya habari ambao ulijikita kuelezea masuala ya uchumi.

Mbowe amesema Tanzania imegeuka kituko baada Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuipatia kampuni ya Acacia ankara ya malimbikizi ya kodi yanayozidi Sh400 trilioni.

"Serikali iziweke hadharani ripoti zote za madini ili kila mtu asome na kujua kuna nini kwenye ripoti hizo. Kiasi cha kodi wanachodaiwa Acacia ni bajeti ya Tanzania kwa zaidi ya miaka 20. Hiki ni kituko," amesema.

Mbowe amesisitiza kwanza chama chake ndicho kilikuwa cha kwanza kudai mabadiliko katika sekta ya madini lakini kile kilichofanywa na serikali hakilingani na mabadiliko ambayo waliyapendekeza.

Akifafanua, amebainisha kuwa mabadiliko yaliyofanyika bungeni yamefanyika kwa papara na hayatalinufaisha taifa.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Yaani huo ni ukichaa kutoka kwa kina Mbowe hadhara gani wanayoitaka kutoka ripoti ya Madini wakati watanzania wote walijionea mubashara wakati wa kusomwa kwake. Wazee kupinga kila kitu hata kile kisichostahiki kupinga.

    ReplyDelete
  2. Mbowe...!!! Kama unasomeshewa watoto Wako na kilipiwa nyumba Ughaibuni. Kwa hili Koma.. Tena ukomeke.. Usijiingize kama uliloahwa na hawa magumashi aksasia. Na hii imekula kwetu na ujio WA Barrick Ni kwamba mazungumzo yanaanza kama Ni ya laki moja au milioni moja wewe chukua likizo ukaangalie wanao. Huna hata staha ya kufunga mdomo Wako wakati taiga na serikali yake ikitutea na Mali asili zetu

    ReplyDelete
  3. Serikali imetakiwa kuweka hadharani!??????
    Na Nani?
    Kitu gani?
    Kwa minajili gani???
    Naomba nirleweshwe. Manake huwa sielewagi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sawa kabisa mdau. Watueleweshe manake vichwa na maudhui vinaoingana kabisa. Sasa hili chama cha nani? Edo amepiga mbizi na kisu hivyo hivyo na mtowe ndiyo njeeee. Na kuanza kutafuta kiki za mitandao. Muulize yule nanihiii....nani vile?

      Delete
  4. Kwa jinsi misukosuko na mbwimbwi zilizotokea kuhusu hilo jambo namuunga mkono mbowe. Hili jambo lilipelekwa Bungeni. na Wapinzani wameteswa, wamewekwa ndani, wameitwa matumbili, wengine wamefariki, wemgi wamepoteza kazi zao. Si jambo la CCM. Ni jambo la Taifa. Na kama Bunge lilipewa rusa kuangalia, kupitisha mswada wa haraka, Inakuwaje tena CCM wanalimaliza wenyewe gizani. CCM watoe mkutahasari wote, makubaliano yote, na imekuwaje warudi bila Raisi magufuli kuinuka na kulieleza Taifa hatma zote. Ndo maana Raisi na Chama cha CCM ni adui halisi wa maendeleo ya nchi hii. Kuna mambo mengi yananishangaza , Watanzania wenzangu inakuwaje mnakubali kuchezewa namna hii. Uhuru, Uzalendo, uwazi, kwa Kanuni na misingi ipi CCM inaliendesha Taifa letu. Kwa namna gani Wasomi wote nchini mpo kimya kwa hili. Sijui mmeridhia au waoga. Hawa wazungu kundi zima lipo kama maaskari, hivi kuna wanaCCM ambao shupavu kuongea na kuafikiana na hawa watu, na kwa nini wawe wanaccm kwa maswala makubwa ya taifa kama haya? Toka Nyerere ajiuzuru, sijamuona Raisi kweli, Mpenda watu na anayejiheshimu mwenyewe na kuwaheshimu Watanzania hata.Sijamwona bado raisi yeyote mwenyehekma na busara hata, Sijamuona raisi yeyote mzalendo halisia dhidi ya maneno la hasha.Hii mikataba kuna usiri mkubwa ndani yake unaowahusisha si maraisi wa Tanzania tu, na maraisi wengine wa nje waliopita ndio maana inakuwa vigumu hata Raisi magufuli kutenda haki. Namuomba Raisi Magufuli amuombe Mungu awe shujaa kamili kutetea mali za maskini wa Taifa hili kama anavyozungumza. Aonyeshe kwa vitendo halisia. Mnayoyaficha hadharani Mungu atayatoa, sababu sauti za Watanzania waliokufa, mliowaonea, waliokufa kwa madhara ya uchimbaji kupitia maji wanayokunywa, utajiri walioukalia wakatimuliwa bila fidia, na kuwapa matajiri wa nje. Vilio vyao hamtaweza kuvifunika hata. Vitawafuata popote, kila wakati hata mkutanapo na hawa matajiri kwa usiri. Mbele za Mungu hakuna usiri. Nanyi Watanzania mnaozidi kuunga mkono, Wapinzani walisema, angalieni vizuri mnapigwa maneno matupu, lakini mtashindwa kupata haki zenu sababu ya kukurupuka na hali ndio hii kukurupuka kwa Viongozi wa CCM bado hakujatuletea faida nchini hata. Hawa Wazungu wasingepata faida Wangeondoka. Wajinga, na Wapumbavu ndio waliwao. Ule upumbavu aliousemea ndugu Mkapa ndio huu. Tunauzwa tunashangilia.Sijui tutaamka lini.Hivi kweli hatuna wasomi wakaungana na kuweka timu kama yao wakakaa kwa heshima Watanzania tukafaidika na mali zetu ambazo ni haki zetu. Tunatatizo gani?Hatujiamini? Lini tutajiamini na kudai haki zetu.Vijana hizi ni mali zenu ambazo zingewasaidia sana kuinua uchumi wa nchi hii. Kuleata Ajira, Kujenga mahospitali makubwa badala ya Wachache kukimbilia ulaya, Mngeyamiliki na kumiliki hii migodi wenyewe mkawa mabilionea na kuliinua Taifa. Mtabaki mnaachiwa mashimo matupu, Magonjwa kwenye maji yatakayowaathiri watoto wenu milele. Hawa viongozi wetu wameshajiwekea hzina zao nje. Mkiwa na uchungu mtasimama pamoja na wapinzani kupigania haki zenu. Mkijitosa. Au mtazidi kuwapigia makofi kwenye majukwaa mkiwa mnapumbazwa. Inafia Wakati mjitafakari upya.

    ReplyDelete
  5. apambane na khali yake ..riport imsaidie nn yeye

    ReplyDelete
  6. Hahahaha! piiipooozz pwaaa! Chadema hadi huruma masikini......watasema nini sasa?? Hawana-jipya, hawana-cha-kusema, yooooote JPM kayamaliza, wamebaki 'kukurupuka' na kudandia agenda zisizowahusu......mara waingilie mgogoro wa CUF, mara huku mara kule, kama kawaida yake mzee wa kubadilishia gia angani aka 'MWENYEKITI WA MAISHA'........yakwao yanawashinda mfyuuuuuu.......poleni sana chadema, hebu fanyeni yenu, mumuwache JPM wetu....HAPA KAZI TU!

    ReplyDelete
  7. Kwa Jamani...mti akianza kudata huea anakunali? Hata ukimwambia si ataona unamdhalilisha na atakuina mbaya.. Sasa huwa runamjuaje mtu akiwa anaanza hali hiyo..??? SI kutokana na mane I yake na kubadilika kwa tabia. Je kunatofauti gani na huyu kijana WA zamani... SI ndiyo dizaini ile ile.. Mpaka ukipondukia ataanza kujifungia ndani..hapo ndiyo ita idi tumsaidie hapo kimfokosha MIREMBE Ili aweze kupimwa kwa kina na kuanza majibabu bila kuchelewa..we care for u...Hapa kazi Tu. Chini ya Mkuu JPJM. UTAKE USITAKE. POLE SANA ..SERA HUNA BA AJENDA IMELUPOGA CHENGA. WE NA MAKANIKIA WAPI NA WAPI MKWEPA KODI WETU.. NILIPITA PALE KUKO FLET. KODI UTALIPA TU. USIJIBABAISHE UKAFIKIRI NA SISI PUNGUWANI..SHAURI YAKO KIJANA..SPODI HII HUIWEZI NA WENZAKO WANAKUHUJUMU BILA WEWE KUTAMBUA..AMKA....!!!! ULIWAKARIBISHA MWENYEWE WANAKUAHINDA SASA.

    ReplyDelete

Top Post Ad