DAVIDO Aweka Ngumu Kupost Wimbo Aliyoshirikishwa na Joh Makini Instagram....Joh Makini Afunguka Haya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Msanii wa hip hop Bongo, Joh Makini amesema Davido kutokuonyesha ushirikiano kwa kupost Instagram ngoma yake mpya ‘Kata Leta’ aliyomshirikisha ni kitu ambacho hakiwezi kumuumiza kwa sababu kolabo na msanii huyo wa Nigeria hakuitafuta.



Hata hivyo Rapper huyo kutoka kundi la Weusi ameshangazwa na wanaokomalia suala hilo kwani Davido alipost ngoma hivyo katika mtandao wake wa Twitter.

“Sidhani kama kwangu ni big issue kwa sababu wimbo ni wangu and the end of the day mimi siwezi kujizuia kwa sababu kolabo na Davido sikutafuta, umenisoma?, ilikuja, singeweza kusema siwezi kufanya kolabo na wewe kwa sababu am not sure kama itaipa support,” Joh Makini ameiambia Planet Bongo ya EA Radio na kuongeza.

“Labda mimi nimepigana kupata hiyo kolabo ningeumia nimepigana kupata kolabo halafu jamaa hakuonyesha ushirikiano. Lakini mimi ninachoangalia ngoma ni yangu nimemshirikisha yeye, that’s it,” amesisitiza Joh.

Joh Makini ni msanii wa pili kutoka kwenye Bongo Flava kufanya kolabo na Davido baada ya Diamond Platnumz kufanya hivyo mwaka 2014 alipomshirikisha staa huyo wa Nigeria katika remix ya ngoma yake ya My Number One.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad