Harmorapa: Kwa Sasa Sina Mawasiliano Mazuri na P Funk,

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Harmorapa: Kwa Sasa Sina Mawasiliano Mazuri na P Funk,
Msanii wa hip hop bongo Harmorapa, amefunguka juu ya kitendo cha kumchana mtayarishaji wa muziki ambaye iliaminika anamkubali zaidi, na kukiri kuwa kwa sasa hayuko vizuri na P Funk.

Akizingumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Harmorapa amesema kwa sasa hawana mawasiliano mazuri na P Funk, kwani kuna mambo ambayo yalitokea, yaliyosababisha kutoelewana kwao,

"Nikimzungumzia Majani, kwenye maisha mtu unapitia sehemu nyingi, mfano mimi nafanya kazi kwa mtu halafu maslahi siyaoni, nafanya kazi kwa jasho najituma halafu yeye ndiyo ananufaika, halafu anakuona wewe humfai, na mwisho wa siku ndiyo inakuwa hivyo”, alisema Harmorapa.
Harmorapa kwa sasa ameachia wimbo wake ambao umeonekana kumchana P Funk Majani  ambaye alimsimamia kwenye kazi yake ya Nundu, na kumuunganisha na baadhi ya watu ili aweze kufanikisha kazi zake za muziki.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hamolapa bado tuko njiani anatafuta njia sahihi. ataduka tu. mbona dai alimpa ofa ula iyubo aliingulia kati. ote si chinga ru hamnaiI na na yule alietoka na tunzo kwa obmaa

    ReplyDelete

Top Post Ad