Masikini Mwanaume Auwawa kwa Kupigwa Kisa Kuku

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Masikini Mwanaume Auwawa kwa Kupigwa Kisa Kuku
Mwanaume mmoja mkazi wa kitongoji cha Busulwa kata ya Ngulla Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza ameuawa na kikundi cha watu wasiyojulikana kwa kosa la kuiba kuku watano wa Ester Robert ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Ngulla.

Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, DCP Ahmed Msangi amemtaja mwanaume huyo kuwa ni Leonard Mathias (23) ambapo kabla ya kuuawa alipigwa fimbo na mawe sehemu mbalimbali za mwili wake kisha kuchomwa moto hadi kupoteza maisha na kikundi cha watu wanaojichukulia sheria mkononi mnamo tarehe 21.08.2017 majira ya saa 2:45 asubuhi.
Inasemekana kuwa marehemu aliiba kuku hao nyumbani kwa Bi. Ester kisha kukimbia nao kijiji cha jirani cha Mwabomba ambako huko mwananchi walipomuona walipata mashaka kisha kumkamata na baadaye kutoa taarifa Kijiji cha Ngula ndipo mwenye Kuku alipofika na kukabidhiwa kuku wake.

DCP Msangi amesema mara baada mwenye mali kupokea Kuku wake, wananchi walimchukua na kwenda naye kituo cha Polisi lakini wakiwa njiani walianza kumshambulia kwa kumpiga kwa fimbo na mawe sehemu mbalimbali za mwili wake na baadae kumchoma moto. Polisi walipata taarifa kutoka kwa raia wema ndipo walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo na tukio na kufanikiwa kuwakamata watu saba ambao wanadaiwa kuhusika kwa namna moja ama nyingine katika mauaji hayo.

Jeshi la Polisi linaendelea na mahojiano ya watuhumiwa hao na pindi uchunguzi utakapokamilika kishha ikithibitika kuwa walihusika katika mauaji hayo watafikishwa Mahakamani
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad