Emanuel Okwi Apewa Tuzo ya Mchezaji Bora

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Emanuel Okwi Apewa Tuzo ya Mchezaji Bora
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limemchagua mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi kuwa mchezaji bora wa mwezi wa Agosti katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo yanaendelea kutimua vumbi katika viwanja mbalimbali.

Taarifa hizo zimetolewa na Shirikisho hilo mchana wa leo na kusema wamefikia hatua hiyo baada ya Okwi kuwashinda wenzake wawili ambao ni Mohamed Issa (Mtibwa Sugar) pamoja na Boniface Maganga (Mbao FC) katika uchambuzi uliofanywa Jijini Dar es Salaam jana (Jumatano) na Kamati ya Tuzo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutokana na mapendekezo kutoka kwa makocha wa viwanja mbalimbali ambavyo ligi hiyo inachezwa.
Kwa mujibu wa TFF wachezaji wawili ambao walikuwa wanashindana na mchezaji Okwi kutoka Simba timu zao zilifanikiwa kushinda katika michuano ya Ligi Kuu kwa michezo iliyopita round ya pili.

Kwa upande mwingine, timu ya Simba itashuka dimbani Septemba 17 (jumapili) kuivaa Mwadui FC katika kiwanja cha Uhuru Jijini Dar es Salaam.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad