Mchungaji Gwajima Kufanya Maombi ya Kuombea Afya ya Tundu Lissu Kesho

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mchungaji Gwajima Kufanya Maombi ya Kuombea Afya ya Tundu Lissu Kesho
Mchungaji Josephat Gwajima  wa kanisa la Ufufuo na Uzima amefunguka na kusema kuwa siku ya Jumapili atafanya maombezi maalum kwa afya ya Mbunge Tundu Lissu ambaye juzi alipigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa Dodoma nyumbani kwake.

Mchungaji Gwajima amesema kuwa atatumia misa hiyo kulaani vikali kitendo cha kinyama alichofanyiwa Tundu Lissu na watu hao wasiojulikana ambao waliweza kupiga gari lake zaidi ya risasi 30 huku risasi tano ndizo ziliweza kumjeruhi Mbunge huyo.

"Jumapili hii  Septemba 10, 2017 nitaongoza maombi maalumu ya kuombea Afya ya Mhe. Tundu Lissu na kulaani Vikali kitendo cha Kikatili na Kinyama alichofanyiwa. Maombi haya yatafanyika katika Kanisa la Ufufuo na Uzima, Ubungo Dar es Salaam tunawakaribisha wote watakaopenda kuungana nasi katika maombi haya" aliandika mchungaji Gwajima kupitia ukurasa wake wa facebook

Mchungaji Gwajima amekuwa akilaani mambo mbalimbali ambayo huwa yanatokea katika nchi kupitia misa mbalimbali ambazo huwa anafanyia katika kanisa lake hilo ikiwa pamoja na kuombea taifa amani na usalama.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad