Serikali ya Awamu ya Tano Chini ya Rais Magufuli ni Sikivu- Mgandilwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Serikali ya Awamu ya Tano Chini ya Rais Magufuli ni Sikivu- Mgandilwa
Wananchi wa Kigamboni wakiongozwa na viongozi wa wilaya wamejitokeza na kufyeka pori la NAFCO lililoko kata ya Somangila, eneo ambalo ni hatarishi kwa usalama wa raia. Akiongea mara baada ya usafi huo Mkuu wa Wilaya amesema Rais Magufuli ni msikivu

Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe Hashim Mgandilwa alianza kwa kuwashukuru wananchi kwa kuwa watulivu kwa muda wote ambao walikuwa wakilalamikia pori hilo huku serikali ikiwataka wawe na subira wakati taratibu za ufutaji zinaendelea.

"Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli ni sikuvu inayodhamiria kuleta maendeleo kwa wananchi ndiyo maana Rais Magufuli amesikia kilio chenu na kuamua kuifuta hati ya Shamba hili ili liwe mikononi mwa serikali, tuendelee kuiunga mkono serikali na sitaki kuona mtu anafanya siasa katika hili, tufanye kazi" alisisitiza Mgandilwa.

Mbali na hilo Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni amewapa wananchi wiki moja kuanzia leo kuendelea kusafisha eneo hilo kwa kufyeka vichaka na kukata miti kwa matumizi yao ya nyumbani kama kuni au shughuli za ujenzi.

Hata hivyo Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Mhe Dkt. Faustine Ndungulile pia amewataka wananchi kuendelea kushikamana kwa Umoja katika shughuli mbalimbali za maendeleo kwani Kigamboni itajengwa na wote. Pia amewaomba wananchi waendelee kuiunga mkono serikali yao kwani imetatua kero zao kubwa pamoja na Rais Magufuli kuifuta mamlaka ya Uendelezaji wa Mji wa Kigamboni (KDA) ambayo ameipigia kelele kwa muda mrefu bungeni.

Pori hilo ambalo lililosafishwa leo na viongozi mbalimbali wa Kigamboni awali lilikuwa likimilikiwa na mfanyabiashara Yusuph Manji ambaye alishindwa kuliendeleza na serikali kuamua kulichukua.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad