Bwana Harusi Apigwa Risasi Sehemu za Siri Katika Sherehe ya Harusi Yake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Bwana Harusi Apigwa Risasi Sehemu za Siri Katika Sherehe ya Harusi Yake
Bwana harusi nchini Misri amejeruhuwa vibaya kwa kupigwa risasi katikati ya sherehe ya harusi yake.
Bwana harusi huyo aliyetambulika kwa jina la Osman al-Alsaied alipata majeraha mabaya katika sehemu yake ya siri, Kiunoni na Mkononi katikati ya sherehe ya harusi yake ambapo mtu huyo aliyempiga alikuwa anafyatua risasi kama kitendo cha kusherehekea harusi hiyo .

Osman al-Alsaied (28) alikuwa akisherehekea harusi yake ndipo mwanaume mmoja alikosea kufyatua risasi badala ya kuelekeza juu silaha hiyo yeye alielekeza chini na kumjeruhi bwana harusi.

Maafisa wa polisi mjini Cairo wamethibitisha taarifa hizo kwa kusema kuwa bunduki hiyo ilifyatuliwa mwananume mwenye umri wa miaka 26 .

Hata hivyo, Polisi  wamesema kuwa mtuhumiwa huyo aliyefyatua risasi alikamatwa na kuhojiwa muda mfupi baada ya tukio hilo kutokea.

Tukio hilo limeibua mijadala mingi kwenye mitandao ya kijamii nchini Misri wengi wakitaka tamaduni hiyo ifutiliwe mbali.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka mtandao wa BBC zimeeleza kuwa bwana harusi huyo anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo na tukio hilo limetokea wiki iliyopita.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad