Nassari Aliamsha Dude Amwita Hussein Bashe Mnafki

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Nassari Aliamsha Dude Amwita Hussein Bashe Mnafki
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari  (CHADEMA) amemvaa Mbunge wa Nzega Mjini, Mh. Hussein Bashe (CCM) kwa kumpachika sifa ya unafiki baada ya kutoa kauli ya kwamba hoja zilizojadiliwa bungeni siku ya jana zinaashiria kuligawa taifa.

Kilichomfanya Nassari kutumia kauli hiyo ya unafiki kwa Hussen Bashe ambapo amejumlisha pia ni sifa ya Wana CCM ni kutokana na Mbunge Bashe kupitia ukurasa wake wa Twitter kusema kwamba amepata hofu juu ya taswira ya viongozi badala ya kujadili mambo kwa msingi ya hoja na kuanza kujadili ukanda.
"Mh. Bashe aliandika "Bungeni Leo nimeona Un holly discussion ambayo imejaa dhana ya kuligawa Taifa kwa misingi ya Ukanda na Ukabila. CCM,Chadema,Cuf na NCCR tuliomo ndani ya Bunge hatuna haki yoyote ya kuanza kupandikiza mbegu ya kuligawa Taifa". 
Ameongeza "Tanu, CCM toka 1957 mpaka leo ilihimiza Umoja na Utaifa na kukemea uhalalishaji wowote wa kuligawa Taifa kwa Misingi ya Dini ukanda na ukabila" Maombi yangu kwa wananchi wenzangu msivumilie mwanasiasa yoyote yule ikiwa ni pamoja na mimi atakayekuja na hoja yenye lengo la kuwagawanya" Bashe
Baada ya mfululizo wa hoja hizo kwenye ukurasa wa Bashe , Nassari leo amejibu hoja hizo kwa kumwambia Mbunge huyo kwamba baada ya yeye kushindwa kumkemea Mwenyekiti wake kwa kutoa kauli zinazotafsiriwa kuwa ni za kibaguzi ndipo anaibuka na kusema taifa linagawanywa.
"Unafiki ni moja wapo ya sifa kubwa ya mwanaCCM,  HusseinBashe ulishindwa kumkemea mwenyekiti wako wa chama akitoa kauli za kibaguzi kanda ya ziwa juu ya bomoa bomoa, leo wanaibuka wabunge kukemea ndio unajitokeza na kusema tunaligawa taifa?!" Nassari.
Ameongeza kwamba "Kunyamazia uovu huu kwa kujifanya hatuuoni sio kulisaidia taifa, ni vyema na ni wakati sahihi kukemea kabla halijamea".

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wewe naseru Na biashara yako ya kuuza filashi. Soko limedirora filasgi za Kuchina hazina Soko.
    Alicho zungumza Bashe Ni sawa kabisa Na ndito mlicho dhihirisha .
    Tanzania Ni yetu Na susi hatukubali Na wala hatuto kubali kuliona mnataka kutuchezea.
    Kwa mwenye kujua Na mwelewa nzuri. Hizi mbinu zenu za long term achievement HATUZIKUBALI NA WALA HATUTO NGOJA MPAKA ZIOTE MIZIZI. WE WILL KILL BEFORE IT GROWS.
    NA KAMA NDIYO IMANI ZENU NI UAMSHO WA KULIGAWA TAIFA.
    BASI MSAHAU HAITO TOKEA.
    NILISTAAJABU SANA HATA NWENYEKITI WENU ALIVYOKUWA AKIYLIZA MASQALI YAKE WITH HUDDEN AGENDA.
    LAKINI KAMPATA MH. J.MAJALIWA HE IS WIDE AWAKE AS WE ARE.

    ReplyDelete

Top Post Ad