Njombe Mjini Yasajili Nyota Wawili Waliyoshiriki AFCON U17

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Njombe Mjini Yasajili Nyota  Wawili Waliyoshiriki AFCON U17
Klabu ya Mtibwa Sugar imewaruhusu nyota wake wawili Nickson Clement kibabage na Muhsin Makame Malima kujiunga na kikosi cha Njombe Mji kwa mkopo wa miezi sita.

Mchezaji wa klabu ya Mtibwa Sugar na timu ya Taifa ya Serengeti Boys, Muhsin Makame Malima

Nickson Clement Kibabage anayemudu kucheza mlinzi wa pembeni na Muhsin Makame Malima anacheza nafasi ya kiungo mshambuliaji na mshambuliaji wamejiunga na kikosi cha timu ya Njombe Mji kutoka katika mkoa wa Njombe.

Kwa takribani wiki moja wachezaji hawa wa kikosi cha Mtibwa Sugar walikuwa katika majadiliano na uongozi wa Njombe Mji na hatimaye makubaliano yamefikiwa na pande zote tatu ambazo ni wachezaji wenyewe , Klabu ya Mtibwa Sugar na Njombe Mji.

Wachezaji hawa waliokuzwa katika Academy ya Mtibwa Sugar yenye mskani yake Manungu wamejiunga na Njombe Mji kwa mkopo wa miezi 6 hivyo wachezaji hawa watadumu katika kikosi hicho hadi mwisho wa msimu huu wa 2017/2018.

Muhsin Makame Malima na Nickson Clement Kibabage ni kati ya vijana waliowakilisha taifa katika michuano ya AFCON chini ya miaka 17 kwa mara ya kwanza.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad