Vanessa Mdee Apewa Tuzo Maalum ya 'Nyota wa Mchezo'

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Vanessa Mdee Apewa Tuzo Maalum ya 'Nyota wa Mchezo'
Vanessa Mdee amekuwa msanii wa kwanza Tanzania kupokea Plaque ya ‘Nyota Wa Mchezo’ baada ya kutajwa kwenye vipengele vya  #BestFemaleAct #BestPerformer #BestLiveAct #EmergingArtistOfTheYear.
Plaque hiyo inatolewa na kipindi cha The Playlist cha Times FM na mtangazaji Omary Tambwe aka Lil Ommy kwa kutambua mchango na mafanikio ya msanii na kazi nzuri aliyozofanya.

Wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Times FM.

Kwa mujibu wa Lil Ommy, lengo la Plaque hiyo ni kuwapa nguvu na kusherehekea mafanikio ya kazi za msanii na sanaa kwa ujumla Tanzania.
“Wazo la kumtambua na kumtunuku ‘Nyota wa Mchezo’ lilianza Disemba mwaka jana tarehe 18 ambapo nilitumia twitter kutaja wasanii wengi kama ‘Nyota wa Mchezo’ kuwatambua waliofanya vizuri kwenye sanaa ya muziki wa kizazi kipya,” amesema Lil Ommy.


“Vanessa alikuwa ni miongoni mwa mtu wa kwanza kuandika tweet yake na wazo lilianzia baada ya kumfikiria yeye na kuona kazi nzuri alizofanya na baadae nikaendeleza orodha ya watu wengi kwa hashtag ya #BongoFleva2017 #NyotawaMchezo na kutaja nafasi zao (vipengele) ambavyo wamefanya vizuri,” ameongeza.

Vee Money na tuzo yake.

Mtangazaji huyo ameeleza kuwa aliangalia impact (matokeo/athari) ya msanii, impact ya kazi zake, popularity (umaarufu), kujulikana, airplays (kazi yake kuchezwa kwenye Radio na TV), Views (watazamani kwenye YouTube), anavyozungumziwa kwenye mitandao ya kijamii, ubora wa kazi, ukuaji wa msanii, ukomavu wa msanii na kuwataja kama NYOTA WA MCHEZO.

Amesema Januari 22 mwaka huu (jana) alim-surprise Vanessa Mdee baada ya kufanya naye mahojiano maalum wakiichambua albam yake bora kabisa ya kwanza na ‘nzito’ ya Money Mondays, kisha kufanya makabidhiano maalum ya Plaque hiyo kutokana na kazi yake katika ofisi za Times FM, DAR ES SALAAM, Tanzania.
Naye Vee Money alionesha furaha yake kwa plaque hiyo kupitia kwenye akaunti yake ya Instagram, akiitaja Jumatatu kama siku yake nzuri zaidi.
“Asanteni Sana Sana Sana…Leo nimezawadiwa tuzo ya Playlist Nyota wa Mchezo 2017. #BestFemaleAct #BestPerformer #BestLiveAct #EmergingArtistOfTheYear.
“Mondays are my FAVORITES 😍 just received a plaque from @timesfmtz Playlist MVP of the year 2017. Asante Sana @lilommy 😍😘💜 album link in my bio,” Vee ameandika kwenye Instagram.
Lil Ommy ambaye anatajwa kushika nafasi ya kwanza katika  watangazaji watano waliofanya vizuri zaidi mwaka jana, na kutanjwa kama MTANGAZAJI BORA WA KIUME Bongo, amesema lengo lake ni kuhamasisha kiwanda cha burudani Tanzania kutambua kazi za wasanii na kusapoti sanaa kama kiwanda kinachotoa ajira kwa vijana na kuchangia pato la Taifa.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad