Zari Kimyaa!... Sasa ni Vita Mpya ya Tunda na Mobetto

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Zari Kimyaa!... Sasa ni Vita Mpya ya Tunda na Mobetto
Ubuyu wa mjini kwa sasa ni vita mpya kati ya mwanamitindo, Hamisa Mobeto na mwanadada anayeuza nyago kwenye video mbalimbali za wasanii wa muziki wa Bongo Fleva, Tunda Sebastian, kisa kikitajwa kuwa ni msanii wa Bongo Fleva ambaye ni baba watoto wa Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Ijumaa Wikienda lina undani kamili.

Chanzo makini cha ubuyu huo kilicho karibu na mastaa hao kilimwaga ubuyu kuwa, wawili kwenye gogoro zito huku Tunda akidaiwa kufanya chokochoko kwa kumrushia vijembe Mobeto ambaye amezaa na msanii huyo ambaye kwa sasa anadaiwa kutoka kimapenzi na Tunda.

Chanzo hicho kilifunguka kuwa, siyo siri tena kwamba Tunda anatoka kimapenzi na msanii huyo anayedaiwa kumpangishia bonge la jumba la kifahari maeneo ya Mbezi-Beach jijini Dar.

TUNDA ADAIWA KUAPA

Ubuyu wa motomoto ulidai kuwa, Tunda ameapa kuwa, lazima mwaka huu amzalie

msanii huyo kama ilivyokuwa kwa Mobeto mwaka jana.

“Mobeto anajua kila kitu kuhusu Tunda kutoka kimapenzi na mzazi mwenziye kwa hiyo kwa sasa ni paka na panya, hawapendani kabisa.

“Hivi karibuni walikutana kwenye sherehe ya mdada f’lani hivi hawakusalimiana, kiukweli huyo msanii wa Bongo Fleva anawachanganya sana wanawake,” kilisema chanzo hicho.


Hamisa Mobeto.

UKWELI NI UPI?

Ili kuujua ukweli wa ubuyu huo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Tunda na kufanya naye mahojiano ambapo mambo yalikuwa hivi;

Ijumaa Wikienda: Habari yako Tunda?

Tunda: Nzuri, karibu.

Ijumaa Wikienda: Kuna habari kwamba kwa sasa unatoka na msanii wa Bongo Fleva, unazungumziaje?

Tunda: Natoka naye tunaelekea wapi?

Ijumaa Wikienda: Yaani unatoka naye kimapenzi na juzikati ulionekana ukila Elements, Masaki.

Tunda: Mtu anawezaje kutoka kimapenzi na kaka yake? Huyo msanii ni kaka yangu na inajulikana na kila mtu, sasa sijui mtu anawezaje kutoka kimapenzi na mtu anayemheshimu kama kaka yake?

Ijumaa Wikienda: Lakini kuna habari kwamba, wewe kuna bifu kubwa kati yako na Mobeto, kisa kutoka na mzazi mwenzake huyo, hilo likoje?

Tunda: Sijawahi kuwa na bifu na Hamisa (Mobeto) ninamheshimu kama dada yangu.

Ijumaa Wikienda: Hivi karibuni kulikuwa na sherehe ya rafiki yenu na mlipokuta wewe na Mobeto mlichuniana, unasemaje?

Tunda: Hilo ndo’ nasikia kutoka kwako.

Ijumaa Wikienda: Je, ni kweli ujauzito ulionao kwa sasa ni wa msanii huyo au unazaa na nani?

Tunda: Nazaa na kaka yangu.

Ijumaa Wikienda: Kaka yako huyo msanii wa Bongo Fleva?

Tunda: (kimya).



TEAM MOBETO NA TUNDA

Kwa upande wa Mobeto alipotafutwa ili atoe neno kuhusiana na ubuyu huo, simu yake ya mkononi iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa SMS hakujibu hivyo jitihada za kumpata ili afunguke anachokijua kwani timu yake imekuwa ikimshambulia Tunda.



ZARI KIMYAAA…

Hata hivyo, tofauti na wengi walivyotarajia kuwa baada ya kuzuka kwa ishu hiyo Zari angekuja juu, yeye amekuwa kimya hadi sasa.



----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad