Mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza Auwawa Kikatili Baada ya Kubainika Kubaka Kisha KumnyongaBinti wa Miaka 12

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza Auwawa Kikatili Baada ya Kubainika Kubaka Kisha KumnyongaBinti wa Miaka 12Mwanafunzi wa kiume mwenye umri wa miaka 15 ambaye alikuwa anasoma kidato cha kwanza shule ya sekondari Gituto katika kaunti ya Murang'a nchini Kenya, ameuawa na wananchi wenye hasira kali, baada ya kubainika kumbaka binti mwenye umri wa miaka 12 na kisha kumnyonga.

Dada wa binti aliyeuawa Grace Kabura, amesema alimuacha mdogo wake nyumbani, na aliporudi hakumkuta.
“Nilirudi nyumbani sikumkuta Wambui, nikawauliza watoto waliokuwa wakicheza jirani wakaniambia ameondoka na Duncan Wakahiu”, amesema dada wa binti huyo aliyeuawa.
Grace ameendelea kwa kueleza kwamba baada ya hapo aliwaomba watoto wamuonyeshe nyumbani kwa kijana huyo na kuwakuta wazazi wake, kisha akawaeleza kuwa anamtafuta mdogo wake ambaye ameonekana kuelekea hapo.
Baada ya hapo wazazi wa kijana wakamuita mtoto wao na kumuuliza mahali alipo mwenzake, akawaambia amemtuma dukani na hajarudi.
Grace ameendelea kueleza kuwa wazazi wake waliingiwa na mashaka na kuamua kupekua ndani ya chumba cha kijana wao, na kukuta mwili wa Wambui ukiwa uvunguni na kijana huyo kukimbia.
Hata hivyo wananchi waliamua kumsaka kijana huyo na walipompata walimshushia kipigo na kumuua.
_________

LOVE STORY YA UTANIKUMBUKA NEYLA Ipo tayari ni maandishi na Sauti !, Kuisoma yote Bonyeza HAPA Lipia tsh 1000 Tu mtandao wowote,au Tembelea www.makapedia.com

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad