Werrason Atua Bongo Kukinukisha Jumamosi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Werrason Atua Bongo Kukinukisha JumamosiWerrason akiwasili fukwe za Escape One na wanamuziki wenzake huku akiongozwa na mwenyeji wao ambaye ni mtangazaji wa Clouds FM, Hamisi Dakota.


MSANII wa muziki wa dansi kutoka  Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Werrason yupo nchini Tanzania kwa ajili ya kufanya shoo Jumamosi hii katika fukwe za Escape One Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Muda mfupi uliopita mwanamuziki huyo alipata fursa ya kuzungumza na waandishi wa habari katika kikao kilichofanyika katika fukwe hizo ambapo amesema hapa nchini anamfahamu Msanii Diamond Platnumz pekee maana amekuwa akimsikia mara kadhaa akitajwa huko Congo.


Werrason na wanamuziki wake wakitoa kionjo cha wimbo kabla ya kuhitimisha kikao na wanahabari.

Hivyo amewaomba wasanii wa hapa nchini  wamtafute kuanzia leo ili wabadilishane mawazo na hata ikiwezekana kufanya klabo ya pamoja kabla ya siku yake ya kufanya shoo yake hiyo ya Jumamosi na ile ya Jumanne katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.


Waandishi wa habari wakichukua matukio mbalimbali ya kikao hicho kilichofanyika katika fukwe za Escape One mapema leo.

“Waafrika ni kitu kimoja hivyo ningependa wiki hii moja ambayo nipo hapa nipate kubadilishana mawazo na wasanii wa hapa Tanzania, ila hata kama kuna mtu angependa tufanye ngoma ya pamoja nipo tayari kwani kufanya hivyo ni kukuza muziki wetu wa Afrika ambapo utapata promo ya nchi nyingi jirani,” alisema Werrason.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ni msanii mkali sana Congo natamani ningekuwa bongo ningeenda kwenye show kumuangalia anazo video kali sana huwa naziangalia

    ReplyDelete

Top Post Ad